Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Bashir Mrindoko (wa pili kulia) akiwa na
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Jackson Midala (wa kwanza kushoto)
walipotembelea eneo la Jangwani
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Bashir Mrindokoleo ametembelea eneo la
Jangwani, Darajani, barabara ya Morogoro kujionea uharibifu mkubwa wa
mabomba ya maji.
Mabomba
hayo ya inchi 16 yenye urefu wa mita 12 yamezolewa na maji kutokana na
atharii liyoletwa na mvua kubwa ya mwishoni mwa wiki inayoendelea jijini
Dar es Salaam.
“Ni
athari kubwa ambayo imesababishwa na mvua hii na mpaka kukata mabomba ya
maji, ni muda mrefu tangu mvua ya aina hii kutokea Dar es Salaam”,
alisema Inj. Mrindoko.
“Nimekuja
kuangalia hali halisi na kuona namna gani tutafanya kufanya ukarabati
wa mabo mba haya, ili kurudisha huduma ya maji kwa maeneo yaliyoathirika
baada ya tukio hili. Tumefanya tathmini na kuona nini cha kufanya na
utekelezaji utaanza mara moja”, aliongeza Inj. Mrindoko.





Post a Comment