Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja(kulia)
akichangia mjadala wakati wa kupitia mapendekezo ya Wafungwa
wanaopendekezwa kuachiliwa na mpango wa Parole kabla ya kufungwa rasmi
Kikao cha 25 cha Bodi hiyo leo Aprili 17, 2014 katika Ukumbi wa Hoteli
ya Charity, Jijini Arusha(kushoto) ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhe. Jaji
Mstaafu Eusebia Munuo akifuatilia mjadala huo.
Wajumbe
wa Bodi ya Taifa ya Parole wakipitia makabrasha yenye mapendekezo ya
Wafungwa watakaoachiliwa na mpango wa Parole kabla ya kufungwa rasmi kwa
Kikao hicho lei Aprili 17, 2014 katika Ukumbi wa Hoteli ya Charity,
Jijini Arusha.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto) akiteta jambo
na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia
Munuo(katikati) mapema leo kabla ya kufungwa rasmi kwa Kikao
kilichofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Hoteli ya Charity, Jijini
Arusha(kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt.
Juma Malewa.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia Munuo(katikati
aliyeketi) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi hiyo mara
baada ya kufungwa rasmi kwa Kikao cha 25 cha Bodi hiyo kilichofanyika
kwa siku mbili katika Ukumbi wa Hoteli ya Charity iliyopo Jijini
Arusha(kulia aliyeketi) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John
Casmir Minja ambaye pia ni Katibu wa Bodi ya Taifa ya Parole(kushoto
aliyeketi) ni Mjumbe wa Bodi, Naibu Kamishna wa Magereza Mstaafu, John
Nyoka.
on Thursday, April 17, 2014
Post a Comment