Akizungumza
na kipindi cha Maskani cha 100.5 Times Fm, kamanda wa Polisi mkoa wa
Pwani, Ulrich Matei ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku na
kwamba kulikuwa na ugomvi kati ya wawili hao huku kijana huyo akimtuhumu
mwanamke huyo kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wengine.
Ameeleza kuwa wakati ugomvi unaendelea, mwanamke huyo alizishika sehemu za siri za mumewe na kuzivuta hadi kuzinyofoa.
Mwanaume huyo alipata maumivu makali na alikimbizwa hospitali ya Mkulanga ambapo alifariki.
Jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo na tayari ameshafikishwa mahakamani akikabiliwa na kesi ya mauaji.



Post a Comment