Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAJAMBAZI YAHUKUMIWA MIAKA 270 JELA HUKO MKOANI MBEYA


court
Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Chunya mwishoni mwa wiki iliwahukumu watu tisa kwenda jela jumla kwa miaka 270 baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa kutumia silaha.
 
Washtakiwa hao ni Samweli Sarehe (40), Bahati Kenson (29), Aulesi Andason (28) na Ayubu Swila (24), wote wakazi wa Mbalizi  Wilaya ya Mbeya Vijijini. 
 
Wengine ni Mathias Simfukwe (31), Pascal Simchimba (27) wote wakazi wa  Kijiji cha Kanga Wilaya ya Chunya, Tegemea Kenya (27) mkazi wa Kijiji cha Mjele, Shukuru Mwakatumbula (27) wa Ifumbo na Maleba Kindagilo (46) wa Lupa, Chunya. 
 
Awali, ilielezwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka wa polisi, Raymond Lukomwa kuwa washtakiwa  wote kwa pamoja walifikishwa mahakamani hapo Desemba 27, 2013 kwa kosa moja la wizi wa kutumia silaha  kinyume na Kifungu cha 287A cha Sheria ya Adhabu, Sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2012. 
 
Alidai kuwa washtakiwa walifanya kosa hilo Desemba 14, 2013 katika eneo la Kasangakanyika ambako waliiba vipimo vitano vya dhahabu vyenye thamani ya Sh58 milioni na fedha tasilimu Sh6milioni, mali ya Paul Sinjale (44) na kwamba katika wizi huo walitumia bunduki aina ya shortgun
 
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Chunya, Desdeli Magezi alisema kwa mujibu wa Kifungu cha Tano (A) (ii) cha Sheria ya Adhabu, Sura ya 90 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 wote kwa pamoja wanahukumiwa kifungo cha miaka 270 na kila mmoja atatumikia kifungo cha miaka 30 jela.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top