Mateso
juu ya mateso! Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Grace Mkondora
mkazi wa Mabibo Farasi, Dar anateseka na uti wa mgongo tangu
alipozaliwa.Grace
(31) anayeishi na mama yake, Mary Liyoya alizaliwa kabla ya muda wake
(Miezi 8) na alipozaliwa alikuwa na uzito wa kilo moja tu.Hali yake ilianza kuwa tofauti tangu akiwa mdogo ambapo alikuwa hawezi hata kucheza wala kuongea chochote.Mama
Grace akisaidiana na mumewe, Flumance Mkondora waliweza kumpeleka Grace
katika hospitali mbalimbali ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Taifa,
Muhimbili pasipo kufanikiwa kupata tiba yoyote.
kati ya
hospitali nyingi walizompeleka walikuwa wakikatishwa tamaa na kuambiwa
mara hawezi kupona tena, wengine wakisema kuwa ameshakuwa tahaira hawezi
kupona milele, lakini kwa hilo mama Grace alipingana nalo na wala
hakukata tamaa na maisha.
Kuna kipindi walishampeleka katika maombi kwenye makanisa mbalimbali lakini hakukuwa na matarajio yoyote.
Alipofikisha
umri wa miaka 20, hali ya Grace ilizidi kuwa mbaya zaidi kwani kwa
kipindi hicho alikuwa akitokwa sana na mapovu mdomoni na kujikunja mara
kwa mara na hata kuongea kwake kulikuwa ni kwa shida zaidi kutokana na
ulimi wake kuwa mzito.
Waliamua
kumpeleka tena katika Hospitali ya CCBRT na alipofikishwa kwa ajili ya
vipimo madaktari walimwambia kuwa umri umeshakwenda hivyo viungo
vimekomaa na hawezi kupata matibabu ya kurekebishwa mgongo.
Baada ya
majibu hayo walimpeleka moja kwa moja katika Kituo cha Masista ambapo
hulelewa watu wenye ulemavu nakumuweka kwa miezi mitatu chini ya
uangalizi wa masista.Mama Grace anasimulia zaidi kuwa baada ya kupita
miezi hiyo waliamua kumchukua mtoto wao na kurudi naye nyumbani mpaka
sasa.
Mpaka
sasa Grace anaishi na wazazi wake akiwa katika wakati mgumu, muda wote
kitandani hajielewi, analishwa chakula, huduma zote za kujisaidia
zinafanywa na mama yake.
Kama umeguswa na unahitaji kumsaidia Grace kwa namna yeyote ile usisite.
Mtumie chochote kupitia namba hizi:
Mama yake, 0765 150 423 Mary Liyoya
Baba yake, 0754 311 940 Flumance Mkondora
GPL
Post a Comment