Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAZEMBE NA AS VITA ZOTE ZA DRC ZAPANGWA KUNDI MOJA LIGI YA MABINGWA, NI VITA YA WEUSI MWAKA HUU

Na Prince Akbar, Dar es Salaam
WAWAKILISHI wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), TP Mazembe na AS Vita wamepangwa kundi moja, A katika Ligi ya Mabingwa Afrika kama ilivyo kwa Esperance na C.S Sfaxien za Tunisia ambazo zipo kundi B pamoja na E.S Setif ya Algeria na Ahly Benghazi ya Libya.
Mabingwa mara tano wa michuano hiyo, Zamalek ya Misri wapo pia Kundi A  na wababe hao wa DRC na vigogo wa Sudan, Al Hilal. 
Vijana wa kazi; Washambuliaji tegemeo wa TP Mazembe, Watanzania Mbwana Samatta kulia na Thomas Ulimwengu kushoto wamepangwa kundi moja na AS Vita ya DRC pia

Mechi zinatarajiwa kuchezwa kuanzia kati ya Mei 16 na 18 na 23 na 25, Juni 6 na 8, Julai 25 na 27, Agosti 8 na 10 na  22 na 24 huku timu zitakazoshika nafasi mbili za juu kwenye makundi zikisonga Nusu Fainali.

MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA:
Kundi A: TP Mazembe (DRC), Al-Hilal (Sudan), Zamalek (Misri) na AS Vita (DRC)
Kundi B: Esperance (Tunisia), CS Sfaxien (Tunisia),
Entente Setif (Algeria) na Al-Ahly Benghazi (Libya).
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top