Na Magreth Kinabo, Dodoma
Serikali
iko katika mchakato wa kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa Ugharamiaji Huduma
za Afya ili kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma za afya za msingi
bila vipingamizi vyovyote vya kifedha.
Hayo
yalisemwa leo na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif
Rashid wakati wa ufunguzi wa kukusanya maoni ya wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii kuhusu mkakati huo uliofanyika
kwenye ukumbi wa Dodoma Hoteli.
“
Serikali imedhamiria kuboresha utoaji wa huduma za afya, moja ya
mkakati wa kufikia malengo haya ni kuwa na mkakati endelevu… ninawaomba
ushiriki wenu katika majadailiano haya ili tuweze kutoka na mapendekezo
yatakayoleta ustawi katika sekta ya afya na hatimaye afya ya watanzania
wote,” alisema Waziri huyo.
Aidha
Dk. Radhid alisema licha ya uchangiaji wa huduma za afya kuanza rasmi
mwaka 1993,ambapo wananchi walitakiwa kuchangia baadhi ya gharama za
afya katika vituo vya kutolea huduma vya umma kupitia Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya, ulianzishwa mwaka 1999 na Mfuko wa Afya ya Jamii ulianza
mwaka 2001 na bima binafsi za afya kuaanzishwa.
“Pamoja
na jitihada hizo, bado rasilimali ni chache wananchi wanaopata huduma
za afya kupitia mifuko mbalimbali ni asilimia ni asilimia 18 tu ya
Watanzania wote,” alisisitiza.
Aliongeza
kwamba,mkakati huo unalenga kuongeza idadi ya watu watakaopata huduma
za afya kwa kutumia mfumo wa bima ili kuwahakikishia huduma
wanazozihitaji.
Aliongeza
kuwa hivi sasa gharama za matibabu ya afya zimezidi kukua na
zitaendelea kukua kuliko uwezo wa Serikali wa kutumia mapato ya kodi.
Alizitaja baadhi
ya sababu za kupanda gharama hizo ni taaluma kubadilika kuwa za kisasa,
madadiliko ya magonjwa , kuongezeka kwa magonjwa yasiyoyakuambukizana,
kuongezeka kwa idadi ya watu.
Alisema
ili kuendana na mabadiliko hayo ni muhimu kuwana angalau hospitali ya
rufaa moja kila mkoa, sita za wilaya, vituo vya afya 40 na zahanati 100.
Alisema
kutokana na hali bajeti ya kutosha inahitajika kila mwaka na kuwa na
njia bora ya kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa na mfumo wa bima.
Kwa
Upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Donan Mmbando alisema
takwimu zinaonesha kuwa asilimia 33 ya Watanzania wanaishi katika hali
duni ya umasikini.
Alisema
pia takwimu zilizopo zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania
hawana uhakika wa kupata huduma za afya kwa sababu ya kutokuwa na mfumo
mzuri wa kugharamia huduma za afya hali inayosababisha baadhi ya
magonjwa kuwa sugu.



Post a Comment