Demokrasia ya Vyama Vya Siasa ya Nchi Hii Haitakuwa, Endapo wafuatao hawataachia ngazi Nafasi zao za Uongozi kwenye Vyama vyao:-
1. Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
2. Freeman Aikael Mbowe
3. Maalim Seif Sharif Hamad
4. Dr. Wilbroad Peter Slaa
5. James Mbatia.
Sababu, Wamebana Demokrasia katika vyama vyao kiasi kwamba hakuna kuhoji lolote na ukithubutu kuhoji Unatimuliwa Chamani. Kwa Tabia zao wamewafanya wanademokrasia vijana David Kafulila, Zitto Kabwe na Hamad Rashid Kubaki kwenye Siasa kwa nguvu tu ya Mahakama na ni kama wamewaondoa kwenye ulingo wa siasa.
Hiyo ni Jinai ya Demokrasia, na Haiwezekani Ivumilike wakati tunahitaji Maendeleo ya nchi kwa kukuza Demokrasia.
Kuna Tetesi kwamba Mh. Mbowe atafanya Mabadiliko ya Baraza kivuli la Upinzani kabla ya Bunge la Bajeti Kuanza ili kwa makusudi ya kuwaunganisha ndani yake UKAWA (CUF na NCCR). Hilo siyo lengo, Lengo Kuu ni Kumfagia Zitto.
Hiyo SI demokrasia na Hatuwezi kwenda sawa. Mbowe acha Unafiki.
Mungu Ibariki Tanzania
Paul C. Makonda
Katibu Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM
on Friday, April 25, 2014
Post a Comment