| Msukuma Toroli Fitina Majuto akiwa Hospitalini Hapo |
| Mtembea kwa miguu Cosmas Peter akiwa hoi hospitalini |
Watu watatu wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya kahama mkoani shinyanga kufuatia ajali ya kugongwa na gari iliyokuwa ikiendeshwa na mkuu wa kituo cha polisi cha wilaya ya Kahama Elias Haway huku mmoja akiwa ameumia sana sehemu ya mguu.
Ajali hiyo imetokea Jana majira ya 1.30 usiku katika barabara itokayo isaka kuingia kahama mjiniu ambapo Haway akiendesha gari yake Toyota Rav 4 lenye namba T 798 BSK alimgonga mwendesha pikipiki.
Watu waliogongwa wametambuliwa kwa majina ya Joseph Malugu (35) mkazi wa Mbulu Bw. Fitina Majuto (20) na Cosmas Peter (21) wote wakazi wa mjini hapa mitaa ya Nyasubi mjini Kahama.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema Haway alianza kumgonga mwendesha bodaboda Bw. Malugu katika eneo la Zahanati ya Igalilimi ambapo watu wenye hasira walimzingira wakimtaka asimame naye akakimbia huku akiwagonga tena waenda kwa mguu wawili.
Wamesema Haway akionekana kuwa amelewa hakutaka kuwatii watu waliyokuwa wakimweleza ndipo alipoondoa gari lake kwa mwendo kasi na kwenda kumgonga Bw. Majuto katika eneo la Mkude ambae aliumia sana kwenye sehemu ya tumbo na kusababisha utumbo kutoka nje.
Shuhuda mmoja Mkulo
Iddy amesema eneo hilo pia Haway hakutaka kusimama na aliendelea na
mwendo kasi ndipo alipokwenda kumgonga mtu mwingine wa tatu Bw. Peter
katika barabara ya eneo la Paradise mitaa ya Nyasubi.
Haway
alipohojiwa amekiri kutokea kwa ajali hiyo huku alisema kuna upotoshaji
mkubwa wa taarifa hiyo kwani yeye ndiye aliyegongwa na mwendesha
pikipiki huyo wa kwanza.
| Mkuu wa kituo cha Polisi Kahama Elias Haway |
Amesema alipotaka kusimama kumwona mtu huyo aliyegonga, aliona watu wameanza kumzonga naye akamua kukimbia kwa usalama wake ndipo alipoweza kuwagonga tena wale wengine wawili.
Mganga
Mfawidhi wa Hospitari ya wilaya ya Kahama Dk Joseph Foma amethibitisha
kugongwa na gari watu hao na wamelazwa katika wodi namba moja katika
hospital hiyo, huku hali zao zikiwa mbaya na kwamba wapo katika
utaratibu wa kumuhamishia Malugu katika hospitali ya Bugando Jijini
Mwanza.


Post a Comment