JOSE
Mourinho amegoma kuzungumzia kuhusu kikosi atakachopanga katika mchezo
wa ligi kuu soka nchini England baina ya klabu ya Chelsea dhidi ya
Liverpool jumapili ya wiki hii katika dimba la Anfield.
Siku
za karibuni, Mreno huyo alikaririwa akisema atapanga kikosi dhaifu
katika mechi hiyo ili kuwapumzisha wachezaji wake nyota kuelea nusu
fainali ya pili ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Atlectico
Madrid jumatano ya wiki ijayo uwanja wa Stamford Bridge.
Mourinho
alipoulizwa kuwa anaidharau ligi ya England mpaka apange kikosi
dhaifu?, kocha huyo, 51, alisema mambo ya timu yake aachiwe yeye.
“Siku zote kuchagua kikosi kitakachocheza ni siri ya kocha, Kama mtu anauliza swali hilo, siwezi kumjibu”.
“Kitu cha msingi ni klabu yangu na mashabiki wetu. Nahita
ji kuilinda klabu na mashabiki wa Chelsea”.
ji kuilinda klabu na mashabiki wa Chelsea”.
“Kama
hatusaidiwi kutimiza ndoto zetu na malengo yetu, basi kuna sababu ya
kutuacha tufanye mambo yetu. Subirini jumapili na mtajua timu
itakayocheza” Alisema Mourinho.
Kocha
huyo wa zamani wa Real Madrid alipoulizwa kama mashabiki wa Chelsea
watafurahishwa na mabadiliko ya kikosi, alijibu kuwa mashabiki wa
Stamford Bridge watakuwa na imani na maamuzi.
Mourinho
alieleza kuwa leo hii hakuwa huru katika mkutano na waandishi wa habari
kufuatia adhabu aliyopewa na chama cha soka cha England, FA baada ya
kumpongeza mwamuzi Mike Dean aliechezesha mechi ya Chelsea dhidi ya
Sunderland na kushuhudia paka weusi wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0.
FA wameyachukuliwa maneno ya Mourinho kama kejeli, lakini yeye anachukuliwa kivingine.
Aliongeza:
“Kila ninapozungumza kuna madhara, hata kama nikisema mwamuzi amefanya
kazi nzuri napewa adhabu, kwahiyo sina uhuru kabisa. Kama mnataka
mkutano mzuri nendeni mkazungumze na FA na sio mimi”.
Pia
Mourinho amethibitsiha kuwa nahodha wake John Terry na mshambuliaji
wake Eden Hazard watakosa mechi ya jumapili na wapo hatarini kuwakosa
Atletico jumatano.
Post a Comment