MSICHANA Atu Gabriel mwenye umri wa miaka 20, mwanafunzi wa Chuo cha Eden Hill kilichopo Kwamfipa wilayani Kibaha mkoani Pwani, amekutwa amekufa chumbani kwa mtu anayetajwa kuwa ni hawara yake, Hafidh Mohammed.
Tukio
hilo lilitokea April 26, mwaka huu na kukusanya umati huku mwanaume
aliyelala na binti huyo akitokomea kusikojulikana.Marehemu anadaiwa kuwa
mwenyeji wa Makambako mkoani Njombe.
Akizungumza
na waandishi wetu juzi Kibaha, mama wa Hafidh ambaye pia ni mjumbe wa
eneo hilo, Zainabu Saidi alisema mwanaye alimweleza kutokea kwa tukio
hilo asubuhi kulipokucha na kabla ya hapo, hakuwa akifahamu kama alikuwa
na uhusiano wa kimapenzi na msichana huyo kwa vile aliyekuwa akimfahamu
ni mwanamke mwingine ambaye alizaa naye.
“Mimi
kwa kweli sikuwa na taarifa yoyote juu ya uhusiano wao na huyu
mwanafunzi, nimeletewa taarifa asubuhi na kijana wangu huku akionekana
kuchanganyikiwa, nimejaribu kumsihi asikimbie lakini imeshindikana,”
alisema mama huyo.
ALIVYOAGA CHUONI
Wanafunzi
wa chuo hicho kinachofundisha masomo ya biashara na habari ambao
walikataa kutaja majina yao waliliambia gazeti hili kuwa, marehemu Atu
aliwaaga anakwenda jijini Dar es Salaam kumuuguza wifi yake aliyelazwa
katika Hospitali ya Amana, Aprili 23, mwaka huu.
Hata
hivyo, walisema uondokaji wake uliwapa maswali mengi kwani tofauti na
walivyotegemea kuwa angebeba mfuko mkubwa wenye nguo za kubadili, yeye
aliondoka akiwa na mkoba wake wa mkononi pekee hali iliyoonesha hakuwa
akienda mbali.
Walisema
siku tatu baadaye walipatwa na mshtuko mkubwa baada ya mlinzi wa
hosteli yao kuwaletea taarifa za kifo cha mwenzao kilichotokea katika
chumba cha mvulana huyo anayeishi jirani.
MAJIRANI NAO WANENA
Majirani
waliozungumza na gazeti hili walisema kwao haikuwa mara ya kwanza
kumuona msichana huyo, kwani mara kwa mara alikuwa akifika pale ingawa
akishaingia ndani hakuwa akitoka nje.
Walisema mara zote hizo, mwanaume huyo mwenyeji ndiye alikuwa akitoka nje na kwenda kumnunulia chakula.
POLISI WAUPELEKA MWILI HOSPITALI YA TUMBI
Jeshi la
polisi liliwasili eneo la tukio na kuukuta mwili huo ukiwa umelala
kitandani ukiwa hauna jeraha, lakini pembeni yake kulikutwa vidonge
ambavyo havikufahamika ni vya aina gani ambavyo pia vilichukuliwa pamoja
na mkoba wake hadi kituonis.
Minong’ono
kutoka kwa majirani kuhusiana na vidonge hivyo ilitofautiana, baadhi
yao walisema huenda vilitumika katika jaribio la kutoa mimba, wengine
walisema inawezekana msichana huyo alipata ugonjwa wa ghafla usiku na
mwanaume huyo alikwenda kumchukulia vidonge hivyo ambavyo havikuweza
kumsaidia marehemu kupata nafuu.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Pwani, SACP Ulrrich Matei alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kusema juhudi za kumtafuta mwanaume huyo zinaendelea huku
madaktari nao wakiendelea na uchunguzi wao ili kubaini chanzo cha kifo
hicho





Post a Comment