Ikiwa ni Siku ya pili tangu Wajumbe wa
Bunge la Katiba Kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo,Cuf na NCCR
Mageuzi wanaounda kitu kinachoitwa UKAWA wasusie Shughuli za Bunge la
Katiba kwa Madai wamechoka Kutukana na Kuburuzwa kwenye Bunge hilo.
Hii leo Naibu waziri wa Fedha Mh:Mwigulu
Nchemba ambaye kwa Sasa anakaimu Kuwa Waziri wa Fedha tangu
Tarehe.10./04/2014 hadi 18/04/2014 kutokana na Waziri wa Fedha kusafiri
Nchini Marekani Kikazi,amefuta Malipo ya wabunge waliosusia Mchakato wa
Katiba.
Habari za Uhakika Kutoka Chanzo chetu ndani ya
hazina kinasema,Mwigulu Nchemba
ameagiza Mabenki yote kurudisha Cheque za Malipo ya Posho na seating
allowance zilizopelekwa na Bunge jana tar.16/04/2014 ili ziwekwe kwenye
akaunti binafsi za Wabunge ikiwa ni Malipo ya Mpaka tar.30/04/2014.Pia
ilikujiridhisha na taarifa hizo,Mwandishi wetu alizungumza na Wajumbe
namna Mtiririko wa Malipo unavyofanyika ndani ya Bunge hilo,Mjumbe(Jina
tunalihifadhi) alisema fedha zote zinapitia Benki na wakati
wanajiandikisha siku za Kwanza walitakiwa Kuandika namba zao za Benki na
Malipo yote hupitia huko,hivyo kama ni fedha zinazuiliwa Benki.
Baadhi ya wabunge wa CUF na Chadema wanaojiita
UKAWA toka jana walijua wameshasaini fedha hizo hivyo zitaingia
kwenye account zao Binafsi. Mambo yamekuwa tofauti baada ya Naibu Waziri wa Fedha(Sera) Mh:Mwigulu
kuagiza leo form zisainiwe upya leo na zitasainiwa pia tar 22
mpaka 25,Kwa madai ya asiyefanya kazi na asile.
Mbali na hilo,Mh:Mwigulu amenukuliwa na
clouds fm akisisitiza Rais kuwafuta wajumbe wakiojitoa na badala yake
awateue watu waliotayari kutunga katiba hata bure kuliko hawa
wanaokutana vikao lukuki kupanga njama za kususia mchakato. Aidha
Mwigulu alisema fedha inayotumika ingeweza kulipwa Wazabuni wanaozidai
halmshauri, wangeweza kulipa madeni ya walimu, au kuwapa mikopo watoto
wa masikini waliofaulu ila hawajaenda vyuo kwa kukosa mikopo, au
zingenunua madawa hosipitalini, au zingepeleka umeme, maji, vitabu au
barabara lakini wamelipwa wajumbe badala ya kufanya kazi hiyo wanapanga
njama ya kuhujumu mchakato usiendelee kwa kutafuta visingizio lukuki.
Bunge la
Katiba linategemewa kuendelea Tar.22 Mwezi huu mara baada ya sikukuu za
Pasaka Kupita na litaahirishwa tena Tar 25 mwezi huu kupisha Bunge la
Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Post a Comment