Mkurugenzi
Udhibiti Ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Tumaini
Mtitu akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mikakati
ya kudhibiti ubora wa bidhaa za ndani na zinazotoka nje ili kuepuka
madhara kwa watumiaji wa bidhaa hizo. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa
shirika hilo Bi Roida Andusamile.
PICHA ZOTE NA FATMA SALUM
…………………………………………………………………………………………….
Na Frank Mvungi-Maelezo
Serikali
imedhamiria kuwainua wajasiriamali wadogo hapa nchini ili kuongeza
uzalishaji wa Bidhaa za ndani zitakazosaidia kuimarisha uchumi wa Taifa.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa Shirika la viwango hapa
nchini (TBS) Tumaini Mtitu wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari leo
jijini Dar es salaam.
Alisema
shirika hilo limekuwa likishirikiana na Shirika la Viwanda Vidogo
(Sido) kuwajengea uwezo wajasirimali wadogo ili hatimaye wazalishe
bidhaa zenye ubora na hivyo kupata cheti cha ubora kinachotolewa na
shirika hilo.
Mtitu
aliongeza kuwa wajasiriamali wote wanaojihusisha na uzalishaji wa
bidhaa hapa nchini wanatakiwa kuthibitishwa na shirika hilo ili
kuwalinda watumiaji wa bidhaa hizo kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora
unaotakiwa kwa mujibu wa sheria.
Aliwataka
Wajasiriamali hao kupitia SIDO ili waweze kujengewa uwezo wa kuzalisha
bidhaa bora na baada ya hapo bidhaa zao ziweze kukaguliwa na kama
zikikidhi vigezo wapate cheti cha ubora ambapo mchakato huo unaweza
kuchukua mwezi mmoja.
Akizungumzia
faida za Wajasiriamali kupata cheti cha ubora baada ya bidhaa zao
kukidhi vigezo vilivyowekwa na shirikika hilo, Mtitu alisema
unawawezesha wajasiriamali kupanua wigo wa soko la bidhaa zao na kuwa
wa kimataifa.
Wakati
huo huo Mtitu aliwataka watanzania wote kufuata taratibu zilizowekwa na
Serikali kupitia shirika hilo ili waweze kupata cheti cha ubora na
kuchangia katika kukuza uchumi wa Taifa.
Utaratibu
wa kupata alama ya ubora ni kwanza kuwasilisha maombi kwa mkurugenzi
Mkuu wa TBS, ukaguzi wa awali na upimaji wa Sampuli za bidhaa husika na
hatimaye kutolewa kwa cheti cha ubora baada ya bidhaa husika kukizi
vigezo.


Post a Comment