Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George Yambesi (kulia) na Afisa
Masoko na Mauzo TTCL Bw. Peter Ngota (kushoto) wakitia saini mkataba wa
makubaliano ya kuweka mtandao mmoja wa mawasiliano Serikalini hivi karibuni
jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George Yambesi (kulia) akibadilishana
Mkataba waliosaini Mkurugenzi wa Kampuni
ya Softnet Gilbert Herman (kushoto)hivi karibuni jijini Dar es salaam .
Mtendaji
Mkuu Wakala ya Serikali
Mtandao Dkt. Jabiri Bakari (kushoto) akiwapongeza makampuni ya
Kitanzania ya TTCL na Sosftnet kwa kushinda zabuni ya kujenga mtandao
wa
mawasiliano na kuyashinda kampuni nyingine duniani. Kulia ni Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma Bw. George Yambesi.
Baadhi ya washiriki
waliohudhuria hafla ya kusaini mikataba ya kuweka Mtandao wa Mawasiliano wa
Serikali kati ya hivi karibuni jijini Dar es salaam. Picha zote na
Eliuteri Mangi-Maelezo
********************************
Na
Eleuteri Mangi-Maelezo
Serikali
imetiliana saini makubaliano na
makampuni yaliyoshinda zabuni ya kujenga mtandao wa mawasiliano.
Makubaliano
hayo yalisainiwa hivi karibuni jijini Dar es salaam kati ya Katibu Mkuu Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George Yambesi kwa niaba ya Serikali
na kampuni ya Softnet Teknology Ltd pamoja na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).
Katibu
Mkuu Yambesi alisema kuwa mradi huo unalenga kuweka mtandao mmoja wa
mawasiliano Serikalini na taasisi zake na unasimamiwa na kuratibiwa na Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (OR-MUU).
“Mradi
huu ni hatua muhimu ya utekelezaji wa Serikali Mtandao ukiwa na lengo la
kuipatia Serikali na taasisi zake mawasiliano ya sauti, data, nyaraka na picha
yenye uhakika, rahisi, salama na yanayopatikana kwa muda wote” alisema Katibu
Mkuu Yambesi.
Akifafanua
kuhusu malengo ya mradi huo Yambesi amesema yanaenda sanjari na malengo ya kujengwa
kwa mkongo wa Taifa na utekelezaji wa sera ya Serikali mtandao, Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003, programu ya mabadiliko ya
utekelezaji wa kazi na utoaji wa huduma katika katika Utumishi wa Umma.
Malengo
mengine ni Mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini (MKUKUTA), Mpango
Taifa wa Maendeleo ya miaka mitano 2012 hadi 2016 na Dira ya Maendeleo ya Taifa
2025.
Katibu
Mkuu Yambesi alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo utazihusu Wizara, Idara
zinazijitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za mikoa na Mamlaka za Serikakali za Mitaa.
Aidha, mkataba huo utazihusisha taasisi 72 ambazo
ni Wizara zote, Idara zinazojitegemea 16 na Wakala 30 zitaunganishwa kwenye
mtandao huo.
Katibu
Mkuu Yambesi alisisitiza kuwa taasisi zilizobaki zikiwemo Sekretarieti za Mikoa
na Mamlaka ya Serikali za Mitaa pamoja na Idara nyingine za Serikali zitaunganishwa
kwenye mtandao huo kwa kutegemea upatikanaji wa fedha.
Naye Mtendaji
Mkuu Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Jabiri Bakari alisema kuwa amefarijika
na ushindi wa makampuni ya
Kitanzania yaliyoshinda tenda ya
kutekeleza mradi huo mara baada ya kuzishinda kampuni nyingine duniani.
Dkt.
Jabiri Bakari aliongeza kuwa mradi huo utaongeza tija na ufanisi katika
utekelezaji wa sekta ya Umma ambapo kutakuwa na mawasiliano rahisi, imara na
uhakika baina yake na wadau wote nchini.
Kwa
upande
wake Mwakilishi wa Kampuni ya
Softnet Nuru Othman aliishukuru Serikali kwa kuwaamini na kuwapa kazi
hiyo na ametoa wito kwa Makampuni ya Kitanzania watumie uwezo wao
kufanya kazi kwa weledi ili kufanya makampuni ya Kitanzania
yatambuliwe
na kuaminika Kimataifa.
Mradi
huu unafadhiliwa na Benki kuu ya Dunia kuptia programu ya miundimbinu ya
“Reginal Communication Infrastructure Program- (RCIP) Tanzania”.
Post a Comment