Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

STEVE NYERERE, BATULI HAPATOSHI


Stori: Gabriel Ng’osha
Staa wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ na mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ wameingia kwenye bifu zito baada ya kutofautiana katika makubaliano ya kikazi.
Yobnesh Yusuf ‘Batuli’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, hivi karibuni wawili hao waliingia kwenye mabishano wakati Steve Nyerere alipokuwa akiandaa filamu yake mpya iitwayo Get Out ambapo alipaswa kumshirikisha Batuli.
Ilisemekana kwamba jamaa huyo alipompigia simu, mwanadada huyo alichomoa baada ya kuona makubaliano ya kifedha hayazungumziwi.
                    Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’
“Batuli alipohoji kuhusu malipo, Steve hakuweka wazi ndipo mambo yalipoharibika, kikanuka kisha Batuli akamvaa kwa maneno kiongozi huyo na kudai hana sifa za kuwa kiongozi,” kilisema chanzo chetu.
Ili kujiridhisha na madai hayo, mwanahabari wetu alimwendea hewani Batuli ambapo alipatikana na kukiri kuwa ametofautiana na

Steve chanzo kikiwa ni filamu hiyo. “Aliponipigia simu nilimwambia sitaweza kwenda kushuti kwa sababu hakuna makubaliano yoyote tuliyofanya ikiwemo gharama, usafiri, mavazi na vinginevyo ndipo akamaindi na kuanza kulaumu na kisha kukata simu,” alisema Batuli.
Ishu haikuishia hapo, taarifa zinadai kuwa baada ya Steve kutofurahishwa na majibu ya Batuli, aliendelea kumtumia meseji za kumlaumu ndipo Batuli alipochachamaa zaidi kwa kujibu mashambulizi.
Staa wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’
“Steve anapaswa akasomee utawala na uongozi bora kwani hafai kuwa kiongozi, hana busara, kwa sababu kabla sijagombana naye nilikuwa nikisikia maneno na majungu ila baada ya ugomvi wangu na yeye nimegundua hafai,” alisema Batuli na kuongeza:“Ananiambia mimi ni msanii mchanga ilihali mimi kwenye kiwanda nipo kwa miaka kumi na nne na mwaka 2,000 wakati naanza yeye alikuwa anachekesha watu ili apate kula kwanza nimemdharau kwa sababu amekuwa akinichonganisha na wasanii wa Bongo Movie eti mimi nimewaambia wanajiuza.”
Baada ya Batuli kufunguka, gazeti hili lilimgeukia Steve Nyerere na kumsomea madai hayo ambapo alifunguka:“Sipendwi na watu na sijui nini tatizo, nikiwa kama dairekta nina uwezo wa kumchagua huyu nifanye naye kazi na huyu kumuacha,

yule (Batuli) kama analeta chuki basi zitakuja hivyo basi ni nyingi tu,’’ alisema Nyerere na kuongeza:
“Kwa heshima niliyoitengeneza kwa miaka 32 alafu nije nigombane na mwanamke, kwanza nagombana naye nini? Nashukuru nimepata ushauri, naendelea na kazi ya kutetea maslahi ya Bongo Muvi kama ni filamu mimi nilishachezesha msanii mwengine.”




 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top