Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Uamuzi wa Mahakama baada ya Mlalamikaji kupinga Biblia kutumika kuapisha viongozi Kenya.


 

Screen Shot 2014-04-18 at 12.46.11 AMPale ambapo alijitokeza jamaa mmoja na kwenda mpaka Mahakamani kupinga kitendo cha Biblia ambacho ni kitabu kitakatifu cha Mungu kutumika kwenye shughuli za kuwaapisha Watumishi wa Umma na kwenye Mahakama kuapisha mashahidi.
Taarifa mpya inasema Mahakama ya upeo nchini Kenya imetupilia mbali kesi hiyo na kusema Mlalamikaji wa kesi hiyo ambae ni David Gitahi hakutoa sababu zozote za kikatiba kulazimu Mahakama kutoa uamuzi wa kuondolewa kwa Bibilia.
Mlalamikaji Gitahi alisema ametumwa na Mungu kushughulikia changamoto na matatizo ya kiroho yanayo kabili taifa la Kenya lakini alipingwa na mwanasheria mkuu wa serikali Githu Muigai aliesema kipengee cha katiba namba 74 kinaeleza ni lazima wakuu katika serikali kuapishwa kabla hawajaanza kazi katika nyadhifa zao tofautitofauti.
Kwenye lalamiko jingine Gitahi alitaka viongozi wa Serikali wasitumie kiapo cha Biblia kwa sababu wanashindwa kutimiza majukumu yao kama walivyoapa na hiyo inabebesha nchi dhambi mbele za Mungu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top