Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Ukawa nusura ‘wamchenjie’ Mbowe



Mwenyekiti wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Freeman Mbowe (kulia) na Mjumbe wa Umoja huo, James Mbatia wakiingia katika Ukumbi wa African Dream mjini Dodoma walipohudhuria mkutano wa wajumbe wa Bunge la Katiba wa umoja huo ambao wamegoma kuendelea kuhudhuria vikao vya Bunge. 
Ni baada ya kuchelewa kuwasili katika mkutano wao, walihofia kugeukwa baadaye aliwasili na kuwaeleza yaliyojiri. Wajumbe wa Mkutano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), juzi nusura wamgeuzie kibao mwenyekiti wao, Freeman Mbowe baada ya kuchelewa kufika kwenye mkutano ulioandaliwa ikiwa ni siku moja baada ya kususia kikao cha Bunge la Katiba.Ukawa walikutana kwenye Ukumbi wa African Dream kwa ajili ya kujipanga baada ya kususia mkutano wa Bunge.Mkutano huo ulioanza saa 4:18 ukiongozwa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba baadaye wajumbe walianza kuhoji walipo viongozi wao, Freeman Mbowe na James Mbatia.Mmoja wa wajumbe wa mkutano huo, Profesa Abdallah Safari alisimama na kuhoji walipo viongozi hao hatua iliyoanza minong’ono miongoni mwa wajumbe wakiwa na hisia kwamba huenda wamewageuka na kwenda kwenye Kikao cha Kamati ya Uongozi.“Tujue kabisa kama wametugeuka...Tumeshakubaliana hakuna mtu kwenda kwenye Mkutano wa Kamati ya Uongozi, sasa kama amekwenda tujue,” ilisikika sauti ya mmoja wa wajumbe.Kuona hivyo, ilibidi Profesa Lipumba aanze kuwapigia simu huku wajumbe wakiwa kimya kusikiliza nini kitafuata. Baadaye Profesa Lipumba aliwaambia wajumbe kuwa ameongea nao wote na wako njiani wanakuja.Baada kusikiliza taarifa hiyo, wajumbe walianza kutoa hoja mbalimbali. Saa 5:07 waliwasili Mbowe na Mbatia kwa pamoja na kwenda kukaa kwenye nafasi zao mbele.Mbowe baada ya kukaribishwa alisema: “Jamani naomba radhi kwa kuchelewa, nilipigiwa simu na Katibu wa Bunge, John Joel kuwa nahitajika kwenye kikao cha Kamati ya Bajeti...Nilikwenda kule kwa kuwa nilijua masuala ya bajeti ni ya kitaifa.“Lakini nilipofika, nikakutana na Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalumu la Katiba, nikawaeleza kuwa siwezi kukaa kwenye kikao hiki, ingekuwa bajeti kama nilivyoelezwa sawa lakini hii nawaambia sitashiriki,” alisema Mbowe na kushangiliwa.Baada ya hapo, Mbowe alieleza msimamo wa Ukawa kuwa hautashiriki Bunge la Katiba hadi hapo utaratibu utakapobadilishwa wa mwenendo wa Bunge la Katiba.Hata hivyo, baadaye Mbowe aliwatoa nje waandishi wa habari akisema wawapishe kwa ajili ya kuzungumza mambo yao ya jikoni
.-MWANANCHI
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top