Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Sixtus Mapunda akiwzungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kushoto ni Omar Said Ng’wanang’waka Mkuu wa Utawala UVCCM
………………………………………………………………………..
Frank Mvungi-Maelezo
VIJANA wametakiwa kujitokeza
kwa wingi kushiriki katika mbio za wazalendo zitakazofanyika Ijumaa
wiki hii ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa
Tanganyika na Zanzibar.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi
(UVCCM) Sixtus Mapunda wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo
jijini Dar es salaam.
Mapunda
alisema mbio hizo zitaanzia Ofisi ya CCM Vijana, Kinondoni hadi ukumbi
wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere uliopo Posta jijini Dar es Salaam.
Alisema
kuwa lengo la mbio hizo ni kuwahamasisha vijana kuweka mbele uzalendo
na maslahi mapana ya Taifa hasa katika kipindi hiki cha Maadhimisho ya
miaka 50 ya Muungano.
Aliongeza
kuwa vijana wanao wajibu mkubwa wa kuuenzi, kuulinda na kuudumisha
Muungano ili kutimiza jukumu lao katika kipindi hiki Taifa linapofanya
mchakato wa kupata katiba mpya.
“Ni
wakati muafaka sasa vijana kuonyesha hilo kwa kushiriki katika mbio
hizo zinazolenga kuenzi na kudumisha Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar”, alisema Mapunda.
Alisema kuwa
kwa sasa vijana wanatakiwa watumie fursa zilizopo katika maeneo yao
katika kujiletea maendeleo kwa kuwa nchi yetu imebarikiwa kuwa na
rasilimali nyingi ambazo zikitumika vyema zitawakomboa vijana”, alisema
Mapunda.
Katika
kutumia fursa zilizopo hapa nchini Mapunda amesema ni vyema vijana
wakajiunga katika vikundi vya uzalishaji mali na hivyo kuweza kunufaika
na fursa zilizopo kupitia umoja wao.
Mapunda
aliwaasa vijana kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ndicho kitu
pekee kinacholiunganisha Taifa hivyo vijana wana wajibu wa kutimiza
lengo hilo.
Post a Comment