WACHEZAJI
wa Barcelona wametembelea eneo maalum lililoandaliwa na klabu kwa ajili
ya kutoa heshima za mwisho kwa aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu hiyo,
Tito Vilanova aliyefariki jana ijumaa. Vilanova aliyekuwa kocha
msaidizi wa Pep Guardiola kabla ya kuwa kocha mkuu amefariki akiwa na
miaka 45 kutokana na maradhi ya saratani ya koo. Baada ya kurithi
mikoba ya Guardiola msimu wa 2012/2013, Vilanova aliiongoza Barcelona
kutwaa ubingwa wa La Liga kwa pointi 100 na kuweka rekodi. Hata hivyo kazi yake nzuri iliingiliwa na maradhi na kulazimika kujiuzulu mwezi julai mwaka jana. Klabu
ilithibitsha jana kuwa Vilanova amefariki na leo hii wachezaji na
makocha wakiwa wageni wa kwanza, wametembelea eneo maalum liliotengwa
kwa shughuli ya kutoa heshima za mwisho kwa Tito.
Sudden: Barcelona's former boss passed away on Friday after losing a battle with throat cancer
Dedication: Members of staff, including Tata Martino conducted a moments silence for Vilanova
Kocha mkuu Gerardo Martino akiwa na mkurugenzi mkuu Andoni Zubizarreta na rais Joesp Maria Bartomeu waliiongoza klabu kutoa salamu za rambirambi. “Baada ya kusaini kitabu cha rambirambi, kikosi kizima kilienda kuitazama picha kubwa ya Tito Vilanova, ambapo walikaa kimya kwa muda kama sehemu ya kutoa heshima kwake”. Barca wameandika kwenye Tovuti ya klabu. “Ilikuwa hali ngumu sana kwa wachezaji kumuona kocha wao aliyewafundisha wengi wao katika soka la ujana na akiwa msaidizi wa Pep na baadaye kuwa kocha mkuu”. Nahodha Carles Puyol alisema: “Kutoka hapa tunatuma salamu za pole kwa familia na marafiki”. Milango ya eneo hilo katika uwanja wa Camp Nou imeshafungulia kwa watu wote kwenda kutoa heshima zao za mwisho kwa Tito
Post a Comment