Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WACHINA WAKAMATWA NA MAKOMBE FEKI YA KOMBE LA DUNIA ZAIDI YA 1,000.

Kama makombe halisi?, mzigo huu umekamatwa katika mji wa Yiwu tayari kwa safari ya kwenda nchini Libya
Maofisa wa kuzuia bidhaa zisizo na hati miliki nchini China wamekamata makombe feki ya kombe la dunia zaidi ya 1,000 katika ghala ya kampuni moja kubwa ya utengenezaji na usafirishaji wa baidhaa
NDOTO ya mashabiki wa timu ya Taifa ya England `Simba watatu` ni kunyanyua kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.

Lakini suala hili limechukua sura mpya na shukurani za dhati ziwaendee viongozi wa desturi wa China waliofanikisha kukamata mzigo feki.

Nchi ya China imekamata makombe feki ya kombe la dunia zaidi ya elfu moja ( 1,000) katika ghala ya kampuni moja kubwa ya usafirishaji nchini humo.

Makombe hayo feki 1, 020 ya kombe la dunia yamekamatwa katika mji wa Yiwu, jimbo la Zhejiang, ambalo ni moja ya miji mikubwa ya usafirishaji wa bidhaa duniani.

Makombe hayo feki kwa asilimia kubwa yanafanana na makombe halisi ya FIFA na yalikuwa tayari kusafirishwa kwenda nchini Libya.

Mkurugenzi wa desturi wa China mwenye mamlaka ya kuzuia nyara zisizohalali alianzisha kampeni mwezi huu wa nne ili kukamata bidhaa zote feki zilizotengenezwa kuelekea kombe la dunia bila kuwa na hati miliki.

Kombe la dunia nchini Brazil linatarajia kuwa na biashara kubwa, na China wameshakamati dili hili na viwanda vyake vimetengeneza bidhaa nyingi za kombe hilo, lakini kuna wajanja wachache wanaotaka kujinufaisha bila ya hati miliki.

Nahodha wa England Steven Gerrard ana matumaini ya kubeba kombe halisi mwaka huu nchini Brazil ambapo wapo kundi moja na mataifa ya Italia, Costa Rica na Uruguay.
Credit:ShaffihDaud
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top