
Mwenyekiti
wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta ametangaza rasmi majina
mengine ya ziada ya wajumbe wapya wa Kamati ya Uongozi ya Bunge hilo.
Majina
hayo yametangazwa leo na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Hassan
Suluhu mjini Dodoma kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa
Bunge hilo.
Taarifa
hiyo ilieleza kwamba Mwenyekiti huyo amefanya uteuzi huo, ili kuleta
muafaka kwa kushirikisha wadau kutoka uwakilishi wa upinzani, ambao
hawakuweza kuchaguliwa kwenye kamati 12 za Bunge hilo.
Makamu
Mwenyekiti wa Bunge hilo aliyataja majina hayo kuwa ni Freeman Mbowe,
Abubakar Khamis Bakari, Fatma Abdulhabib Fereji, Nakazael Lukio Tenga
na Amon Mpanju.
Post a Comment