Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WANAFUNZI WAWILI WAFA WAKATI WAKIOGELEA KWENYE DIMBWI LA MAJI YA MVUA


WANAFUNZI wawili wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Goba, Dar es Salaam, wamefariki dunia wakati wakiogelea.
Wanafunzi hao wametajwa kuwa ni Frank Charles (11) na Videson Peter (11), wote wakazi wa Goba.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi, saa 5 asubuhi wakati wanafunzi hao walipokuwa wakiogelea katika dimbwi la maji ya mvua.
Alisema wanafunzi hao ghafla walizama na kunywa maji mengi na kufariki dunia papo hapo.
Kwa mujibu wa Kamanda Wambura, maiti zote ziliopolewa na wananchi wa eneo hilo na miili yao imehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala.
Wakati huohuo, Askari wa JWTZ kikosi cha Navy Kigamboni, Emmanuel Kamugisha anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 20 na 25, amefariki dunia baada ya kugongwa na gari.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiondo, alisema  ajali hiyo ilitokea juzi, saa 7 mchana eneo la Mgulani, huko barabara ya Kilwa na kuhusisha gari T 141 CVJ Dong Fen iliyokuwa ikiendeshwa na Athumani Kibuda (48), mkazi wa Morogoro.
Alisema dereva huyo aliyekuwa akitokea Mivinjeni kuelekea Keko, wakati akizunguka mzunguko wa Mgulani,  aligongana na  pikipiki  T 428 CKU aina ya Fekon ikiendeshwa na askari wa JWTZ MT Florian Kamugisha ambaye alikuwa amembeba abiria  Emmanuel, wote ni askari JWTZ  Navy Kigamboni.
Alisema katika ajali hiyo, Florian alipata majeraha sehemu mbalimbali mwilini na amelazwa hospitali ya Lugalo. Maiti imehifadhiwa hospitalini hapo, na dereva wa gari hilo anashikiliwa na polisi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top