Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Wanaswa kwa kula maiti ya mtoto

                                      


140414145055 mohammad arif ali 512x288 ikrampiracha nocredit 3731c
Na Hudugu Ng'amilo
Ni visa mbavyo wengi tulivisikia katika hadithi za kale, watu kuliwa na majitu, lakini katika siku za
karibuni tumeshuhudia watu wakila viungo vya wenzao Jamhuri ya Afrika ya Kati katika jazba ya
kulipiza kisasi dhidi ya watu waliowadhulumu katika uongozi uliongolewa mamlakani wa Selekari .


Nchini Pakistan Polisi wamewakamata wanaume wawili kwa makosa ya kuiba maiti ya mtoto kutoka
kaburini na kisha kumla.
Wawili hao Arif Ali na kakake Mohammed Farman Ali waliachiwa huru baada ya kuwa jela kwa miaka

miwili kwa kula nyama ya binadamu.
Hata hivyo wawili hao wameonekana kuwa na tamaa kubwa ya mchuzi wa nyama ya binadamu.
Wakaazi hao wa kijiji cha Daryabn Khan jimbo la Punjab walikamatwa mwaka 2011.
Polisi walisema kwamba walipata kiwiliwili cha maiti ya msichana mdogo kikiwa bila miguu na mikono.
Wawili hai walikiri kwamba walipika mchuzi wa nyama ya viungo hivyo na kuvila.
Walishtakiwa kwa makosa ya kuharibu kaburi kwani nchini Pakistan hakuna sheria inayozungumzia
hatia ya mtu kumla mwenzie.
Punde baada ya kuachiwa nguvuni  Arif Ali alisema kwamba anajutia makosa hayo na kwamba
hatarudia tena.
Hata hivyo punde si punde polisi wamesema waliitwa na majirani ya jamaa huyo wakilalamikia

uvundo mkali kutoka kwenye nyumba yake.
Walipoingia chumbani humo Lo ! wakapata kichwa cha mtoto.
Kiwiliwili hakijulikani kililiwa au kapotelea wapi.
Arif Ali tena amekamatwa kwa mara ya pili na msako unaendelea kumsaka kakake.
Polisi wanaamini ndugu hawa walifukua maiti ya mtoto ambaye kichwa kilipatikana ndani ya makaazi yao.
Wawili hao waliwahi kuoa na hata wakajaliwa na watoto, hata hivyo wake zao waliwatoroka kabla
yao kwenda jela kwa kisa cha awali.(CHANZO BBC)

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top