Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Thabit Mwambungu ameiambia kuwa Serikali ya Mkoa huo imewafikisha
mahakamani wazazi 100 kwa tuhuma za kufanya sherehe baada ya watoto wao
kufeli mitihani.
Pamona na wazazi/walezi hao kujitetea kuwa walikosa karo ya kuwapeleka
watoto hao shule, imeelezwa pia kuwa mazingira duni ya kufundishia na
kujifunza katika Wilaya ya Tunduru, yameelezwa ni moja ya sababu inayowafanya wazazi kushawishi watoto wasisome kwa
bidii wala kufaulu mitihani, ambapo mwanafunzi akifeli mtihani wa darasa
la saba hufanyiwa sherehe.
Imeelezwa pia kuwa wanafunzi wanaosoma katika Shule za msingi Wilayani
Tunduru mkoani humo huambiwa na wazazi wao kuwa wasijaze majibu yaliyo
sahihi wanapofanya mitihani, bali wajaze ‘makorokocho’ ambapo kila
anayefeli mtihani huo hufanyiwa sherehe na Wazazi wake.
Hali hiyo imeelezwa kuchangia kuifanya Wilaya hiyo kuwa ya mwisho Kimkoa na
Kitaifa katika matokeo ya darasa la Saba mwaka jana.
Hali ya Mkoa huo
kielimu nayo hairidhishi kutokana na kuchangiwa kwa mwamko mdogo uliopo
kwa wazazi na walezi.
Post a Comment