Waziri Mkuu na Mgeni Rasmi wa Mkesha wa Muungano
Mizengo Pinda akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kuongoza
mamia ya wananchi waliohudhuria kwenye mkesha huo.Kushoto kwake ni Katibu Mkuu
wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana na kulia kwake ni Makamu wa Pili wa
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Iddi na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhandisi Raymond Mushi.
Wageni waaliwa ikiwemo Mabalozi na Wawakilishi
wa Mashirika za Kimataifa.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya
Utamaduni wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Mwansoko (katikati) akiwa na Katibu Mtendaji
wa Bodi ya Filamu Joyce Fisoo (wa pili kushoto) na watumishi wengine wa Wizara
hiyo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad akiwasili kwenye viwanja vya
Mnazi Mmoja kujumuika katika Mkesha wa Muungano.Kulia kwake ni mwenyeji wake Wilaya ya Ilala Mhandisi Raymond Mushi .
Kikindi cha Taifa cha Taarabu kikitumbuiza
wananchi waliohudhuria kwenye mkesha na wimbo Maalum unaojulikana kama Muungano
Wetu.
Kikundi cha Burudani kutoka Tanga kikuburudisha
hadhira
Mzee Yusuf na Kundi lake la Jahaz Morden
Taarabu.
Baadhi ya vijana wakiburudika
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda, akiwaaga baadhi ya wageni waalikwa na kuondoka baada ya kuongoza Mkesha wa Muungano.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar Balozi Seif Iddi, akitoa salamu zake kwa wananchi.
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda,
akitoa neno kwa wananchi.
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda,
akijiandaa kubofya kitufe cha kuashiria kuzaliwa upya kwa Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar.
Maandishi Maalumu yakihamasishana kuashiria
kutimia kwa Miaka 50 ya Muungano.
Fashfash na fataki zikamiminika kwenye anga ya
viwanja vya Mnazi Mmoja.
Profesa Mwansoko akizungumza na Televisheni One.
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda, akiwaaga
baadhi ya wageni waalikwa na kuondoka baada ya kuongoza Mkesha wa Muungano.
Post a Comment