Wilaya mbili zinatarajiwa kuongezwa na kufanya idadi ya wilaya kuwa
tano katika jiji la Dar Es Salaam. Wilaya hizo ni Kigamboni na Ubungo.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es
Salaam Said Mecky Sadick wakati wa kuhitimisha kikao na baraza la
Mashauri jijini Dar Es Salaam siku ya Jumanne ambapo wilaya ya Kigamboni
itagawanywa na kuwa na majimbo mawili ya Mbagala na Kigamboni.
“Mapendekezo hayo yatafikishwa kwenye serikali kuu na uamuzi wake
utatolewa mwezi ujao’, alisema Mkuu wa Mkoa , ambaye alikuwa mwenyekiti
wa baraza hilo, lililokuwa likijadili pia muswada wa bajeti wa mwaka wa
fedha wa 2014/2015.
Wilaya hizo zitaungana na Manispaa za Kinondoni, Ilala na Temeke za
jijini Dar Es Salaam linalokadiriwa kuwa na watu zaidi ya milioni 4.5.
Loading...
Post a Comment