Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Vedastina Justinian akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Mradi wa Vituo vya Utoaji
Huduma kwa Pamoja Mipakani (One Stop Border Posts) unaolenga kurahisisha
taratibu za forodha, uhamiaji, usimamizi wa ubora wa bidhaa, ulinzi na usalama.
Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Miundombinu ya Kiuchumi Mhandisi Abdillah Mataka
na kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Frank Mvungi.
Mchumi Idara ya Biashara na Sekta za Uzalishaji kutoka Wizara
ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Amedeus Mzee akizungumzia faida
zitakazopatikana kwenye mradi wa vituo vya utoaji huduma kwa pamoja mipakani,
aidha alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na watumishi wa vituo hivyo katika
kuhakikisha mapato hayapotei kwa maslahi ya nchi yetu na jumuiya kwa ujumla.
****************************************
Na Frank
Mvungi-Maelezo
Serikali imejipanga
kukamilisha vituo vya utoaji wa huduma kwa pamoja Mipakani (One Stop Border
Posts-OSBP) vitakavyosaidia kurahisisha taratibu za forodha,uhamiaji,Usimamizi
wa ubora wa bidhaa na huduma ,usalama na ulinzi kwa kutoa huduma hizi upande
mmoja wa mpaka.
Hayo yamesemwa
na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Vedastinian Jastinian wakati wa mkutano na waandishi wa
habari leo jijini Dar es salaam.
Akieleza faida
za vituo hivyo, Vedastinian amesema vitaondoa urasimu uliokuwepo aw
ali na
kuharakisha huduma na kwa wananchi wa nchi wanachama wakati wanapotaka
kusafirisha bidhaa kutoka nchi moja kwenda nyingine.
Alisema Kituo
cha kwanza ni kile cha Holili ambacho kimekamilika na kimekabidhiwa kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ambao
ndio waendeshaji wa vituo hivyo hapa nchini ambapo mradi huu unatarajiwa
kukamilika mwezi Mei 2014.
Alifafanua kuwa
katika mipaka ya Sirari/Isebania unazitenganisha Tanzania na Kenya na kwa
upande wa Mkoa wa Mara mpaka wa Mutukula unazitanganisha Tanzania na Uganda.
Vedastinian alivitaja
vituo vingine kuwa ni Namanga cha Arusha,Kabanga/Kobero kilichopo mpakani mwa
Tanzania na Burundi unatarajiwa kukamilika mapema mwezi novemba 2014.
Alitaja vituo
vingine ni Horohoro Mkoani Tanga na Lungalunga upande wa nchi ya Kenya ambapo
ujenzi wake unatarajia kukamilika mapema mwaka huu.
Mradi huo
unatekelezwa baada ya kutungwa sheria ya jumuiya ya Afrika Mashariki ya kuanzisha
vituo vya utoaji wa huduma kwa pamoja mipakani (OSBP) Katika nchi wanachama wa
jumuiya ya Afrika Mashariki.
Sheria
iliyopitishwa na Bunge la Afrika Mashariki na Iko katika hatua za mwisho za
kuidhinishwa na Wakuu wan chi wanachama.




Post a Comment