Afisa
Muuguzi wa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Ashura Amour Mwinyi, akitoa
maelezo kwa mgeni rasmi Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti wa Wizara ya
Afya Zanzibar Abdullatif Khatib Haji (alievaa shati jeupe), jinsi ya
kuwasaidia watoto kupumua vizuri mara baada ya kuzaliwa. Hiyo ilikuwa
hafla ya kukamilika kwa mradi wa kupunguza vifo vya wajawazito na
watoto vitokanavyo na uzazi – MAISHA, unaofadhiliwa na Shirika la
Misaada ya Maendeleo ya Kimataia la Marekani (USAID), katika ukumbi wa
Hoteli ya Grand Palace Malindi.
Baadhi
ya washiriki wa mkutano wa kukamilisha mradi wa MAISHA kutoka mikoa
yote ya Zanzibar wakimsikiliza Mkurugenzi wa mradi huo Dk. Dunstan
Bishanga (hayupo pichani), akitoa hotuba katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Mradi wa kuboresha Afya ya mama na mtoto Tanzania Dk. Dunstan Bishanga, akitoa hotuba katika mkutano huo. Mwakilishi wa USAID nchini Tanzania Lisa Patel, akitoa maelezo ya mradi wa MAISHA ambao umemaliza muda wake hapa nchini. Mkurugenzi
Mipango, Sera na Utafiti wa Wizara ya Afya Zanzibar Abdul- latif Khatib
Haji akizungumza na washiriki wa mkutano wa mpango wa kuboresha Afya ya
mama na mtoto katika Hoteli ya Grand Palace Malindi mjini Zanzibar. Mkurugenzi
Mipango, Sera na Utafiti wa Wizara ya Afya Zanzibar Abdul-latif Khatib
Haji (katikati waliokaa), wakiwa katika picha ya pamoja ya wafadhili wa
mradi wa MAISHA na wasimamizi wa mradi huo hapa Zanzibar. Wa kwanza
kulia mwenye suti nyeusi ni Mkurugenzi wa mradi wa MAISHA Tanzania
Dunstan Bishanga. (PICHA NA MAKAME MSHENGA- MAELEZO ZANZIBAR).
………………………………………………………………………
Na Makame Mshenga, ZANZIBAR
WIZARA
ya Afya Zanzibar, imesema itahakikisha hatua zilizofikiwa za kupunguza
vifo vya mama wajawazito na watoto wakato wa kujifungua zinakuwa
endelevu ili kufikia malengo ya millennia.
Mkurugenzi
Mipango, Sera na Utafiti katika wizara hiyo Abdullatif Haji, amesema
katika mkutano wa siku moja kufunga mradi wa miaka mitano uitwao MAISHA
uliofanyika katika hoteli ya Grand Palace Zanzibar, kuwa lazima juhudi
za kuimarisha afya ya mama na mtoto ziendelezwe.
Mkurugenzi huyo alisifu hatua iliyofikiwa kwa kupunguza vifo hivyo kutoka 377 mwaka 2012, hadi kufikia 221 kwa sasa.
Amesema
serikali itaendeleza mkakati huo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
ukiwemo mradi wa MAISHA ambao umeweza kusaidia kupunguza vifo hivyo kwa
asilimia 50 katika visiwa vya Unguja na Pemba.
“Lengo letu ni kuhakikisha hakuna mzazi anayekufa wakati wa kujifungua wala kupoteza kizazi chake,” alisisitiza.
Mkurugenzi
huyo alisema mradi huo unaosimamiwa na taasisi ya Jhpiego Zanzibar
chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani
USAID, umesaidia kuwakomboa akinamama kwa kuwaelimisha juu ya umuhimu wa
kujifungulia hospitali pamoja na kuhudhuria kliniki katika kipindi
chote cha ujauzito.
Alifahamisha
kuwa, vifo vya mama wajawazito na watoto vinaweza kupunguzwa na
kumalizwa kabisa, kama kutakuwa na mkakati madhubuti wa utoaji huduma
endelevu na uangalizi wa kutosha kabla na baada ya kujifungua.
Kwa
niaba ya serikali na Wizara ya Afya, Mkurugenzi huyo aliwashukuru watu
wa Marekani na serikali yao, na kwa uzito wa pekee, USAID, kwa msaada
wao mkubwa na muhimu, kwa kufanya kazi bega kwa bega na Zanzibar katika
kuhakikisha vifo vitokanavyo na uzazi vinapungua kwa kiasi kikubwa
Unguja na Pemba.
Alisema
lengo la Wizara ya Afya, ni kuhakikisha vya mama wajawazito
vinavyotokana na uzazi pamoja na vya watoto wanaokufa wakati wa
kuzaliwa, vinapngua hadi 150 ifikapo mwaka 2015.
Mapema,
Mkurugenzi Mkazi wa Jhipiego nchini Tanzania Maryjane Lacoster,
alieleza kuridhishwa na ushirikiano wanaoupata kutoka serikali zote
mbili, ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi Zanzibar.
Alieleza
kuwa, mafaniko yaliyopatikana katika kuokoa maisha ya mama na watoto
wakati wa kuzaliwa, yametokana na msaada na ushirikiano huo katika
mpango huo wa miaka mitano, sambamba na ule wa taasisi nyengine nchini
na zile za kimataifa.
Amesema
mafanikio hayo yameipa moyo Jhipiego kuendelea kufanya kazi kwa karibu
zaidi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, sambamba na washirika
wanaofadhili mpango huo katika kuhakikisha Wazanzibari wanakuwa na afya
bora.
Naye
Mwakilishi wa USAID nchini Tanzania Lisa Patel, aliishukuru Wizara ya
Afya Zanzibar, kwa kuupa ushirikiano mradi huo uliorahisisha wanawake
kupata huduma bora kutokana na vifaa vya kisasa wakati wa ujauzito,
kabla na baada ya kujifungua.
Kwa
upande wake, msimaizi mkuu wa mradi wa MAISHA Dk. Dunstan Bishanga,
alieleza kuwa, tangu kuanzishwa kwa mradi huo mwaka 2008, zaidi ya watoa
huduma 250 Unguja na Pemba, wamepatiwa mafunzo kuhusiana na jinsi ya
kuwahudumia akina mama wajawazito na watoto
Post a Comment