Wastara akifanya usafi ndani kwake baada ya kuolewa.
Na Denis Mtima na Mayasa Mariwata, Pwani
YELEUWII! Kuishi
kwingi ni kuona mengi, kijana aliyejitambulisha kwa jina la Andrew
Vincent (23) ambaye amemaliza kidato cha nne mwaka jana, amejikuta
katikati ya matatizo kufuatia kufunga pingu za maisha na mwanafunzi wa
darasa la tano aliyefahamika kwa jina moja la Wastara (12), wote wakazi
wa Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.Tukio
hilo lilijiri Aprili 26, mwaka huu ambapo kikosi kazi cha Oparesheni
Fichua Maovu ‘OFM’ kilipokea taarifa kutoka kwa wasamaria wema
wakilalamikia kitendo hicho na kutaka mwanafunzi huyo asaidiwe ili arudi
shule.
OFM kama
kawaida yake, ilitinga eneo hilo kwa ajili ya kufuatilia taarifa hizo
ambapo iliweza kuungana na mwalimu mkuu wa shule ya msingi anayosoma ‘bi
harusi’ huyo, Hamad Mnaguzi na viongozi wengine wa kamati ya shule
akiwemo mwenyekiti wa serikali ya kijiji, Shaban Zageni.
OFM na
viongozi hao walikwenda nyumbani kwa wazazi wa mtoto aliyeozeshwa na
kumkuta mama yake aliyejitambulisha kwa jina la mama Wastara huku
akikataa kutaja alikokwenda baba wa mtoto huyo pamoja na wanandoa
wenyewe.
OFM
ilipomuhoji kama anatambua tukio la mtoto wake kuozeshwa alikataa kuwa,
hana mtoto wa shule ambaye ameolewa hivi karibuni huku akidai kuwa yeye
ana mtoto mmoja tu ambaye aliolewa miaka mitatu iliyopita.
Baada ya kubanwa, ndipo akakiri kumuozesha bintiye na kudai kuwa familia ilifanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha.
Hata hivyo, mama huyo akasema hajui makazi ya mwanaume huyo yalipo.
OFM kwa
kushirikiana na viongozi hao wa serikali walimchukua mama huyo hadi
kwenye ofisi ya serikali ya mtaa huo na kumlazimisha aelekeze alipo
mwanae ndipo mjomba wa Wastara alijitokeza na kusema anapajua walipo
wanandoa hao.
Saa 3
usiku, OFM na viongozi hao walifika kwenye kituo cha mafuta kilichopo
Msata, Bagamoyo, Pwani na katika uliziaulizia, nyumba hiyo ilipatikana
ambapo bwana harusi na baba yake walikimbia.
OFM
ilifanya jitihada za kumsaka kijana huyo na kufanikiwa kumnasa na
kumhoji kwa kina sababu ya kuoa denti wa shule ya msingi ambaye walimu
wake wanamtambua kuwa ni mwanafunzi wao, akajitetea kuwa, aliwasiliana
na wazazi wa binti huyo baada ya kukutana naye njiani na kuvutiwa
kumuoa.
“Mimi
sikujua kama mwanafunzi niliambiwa hasomi, najuta! Hapo nimetoa mahari
shilingi 300,000 lakini sina budi kuachana naye,” alisema kijana huyo.
Akaendelea: “Nimelala naye siku moja tu baada ya ndoa, ni vyema wanirudishie mahari yangu.”
Kwa upande wake denti huyo alisema hakuwa tayari kuolewa mapema ila kwa kuwa alikuwa haendi shule akaona bora afanye hivyo.
Baada ya
mahojiano hayo, OFM na viongozi hao walimwamuru binti arudi kwa wazazi
wake ili kufanyiwa mpango wa kuendelea na masomo huku wanandoa hao
wakiangua vilio kwa kuwa ndoa yao ilikuwa bado changa.
na gpl
Post a Comment