STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 30 Aprili, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
amesisitiza umuhimu kwa wizara kutambua vipaumbele katika kupanga bajeti
ili kupata matokeo mazuri.
Alibainisha
kuwa umuhimu huo wa wizara kutambua vipaumbele usaidie Wizara hizo
kuainisha na kuteua miradi michache muhimu katika Mpangokazi wa mwaka wa
fedha ili iweze kutekelezwa kwa mujibu wa bajeti iliyopangwa.
Dk.
Shein alisema hayo jana wakati akifunga mjadala wa Taarifa ya
Utekelezaji wa Mpangokazi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais katika
mfululizo wa vikao vinavyoendelea vya kujadili taarifa za utekelezaji wa
kazi za Serikali kwa kipindi cha Julai 2013 na Machi 2014.
Alifafanua
kuwa malengo ya wizara ndio yanayopanga bajeti na kukumbusha kuwa
mipango mizuri ni ile inayozingatia vipaumbele pamoja na matumizi mazuri
ya rasilimali hivyo suala la kupangaji vyema wa malengo halina budi
kuzingatiwa wakati wote wizara na Idara za Serikali zinapopanga bajeti
zao.
Mhe
Rais aliipongeza Ofisi ya Makamu wa Pili kwa Rais kwa kutekeleza
majukumu yake kwa mafanikio katika kipindi kilichopita ambapo Ofisi hiyo
iliweza kufikia malengo yake.
Hata
hivyo, alitoa wito kwa Ofisi hiyo kutoa elimu zaidi kuhusu Mradi wa
TASAF Awamu ya Tatu ili wananchi waweze kuufahamu vyema.
Mapema
akitoa maelezo ya utangulizi katika kikao hicho Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed alisema katika kipindi
husika Ofisi hiyo imeweza kutekeleza majukumu yake kwa wastani wa
asilimia 79.
Aliongeza
kuwa katika kipindi hicho Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kwa
kushirikiana na Tume ya Mipango na Tume Sayansi na Tekinolojia Tanzania
(COSTESH) ilishiriki katika kuandaa vipaumbele vya utafiti.
Halikadhalika
alieleza Ofisi hiyo imetoa elimu ya kukabiliana na maafa na kuandaa
Mpango wa Wilaya wa Kukabiliana na Maafa pamoja na kuandaa Mazoezi ya
Majaribio(simulation excercises) juu ya namna ya kukabiliana na maafa
ikiwemo mafuriko na ajali za baharini kwa kushirikiana na Shirika
la Chakula Ulimwenguni.
Wakati
huo huo Serikali imesema jumla shilingi milioni 466.2 zimelipwa kwa
kaya masikini Unguja na Pemba katika kipindi cha Januari na Aprili mwaka
huu chini ya Mradi wa TASAF Awamu ya Tatu.
Akiwasilisha
taarifa ya utekelezaji wa Mpangokazi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
Katibu Mkuu Dk. Khalid Salum Mohamed alieleza kuwa kati ya fedha hizo
shilingi milioni 138.2 zimelipwa kwa kaya masikini ya 4054 kisiwani
Pemba kati ya mwezi Januari na Februari na shilingi milioni 155.1
zililipwa kwa kaya masikini 4084 kisiwani humo kati ya mwezi Machi na
Aprili 2014.
Katika
taarifa hiyo, Dk. Khalid alisema kwa upande wa Unguja jumla ya Kaya
2,674 zimepokea msaada kama huo kwa awamu mbili ambapo jumla shilingi
milioni 172.8 zilitolewa.
Katibu
Mkuu huyo alibainisha kuwa Mpango huo wa Kunusuru Kaya Masikini ambao
lengo lake ni kuzisaidia kaya hizo kumudu gharama za elimu, afya na
kuongeza kipato umeonesha mafanikio makubwa ambapo kumekuwepo na
ongezeko la watoto wanaohudhuria masomo kutoka kaya zinazopatiwa msaada
huo.
Dk.
Khalid aliongeza kuwa kumekuwa pia na ongezeko la mahudhurio katika
kiliniki kwa mama wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka 5.
Kuhusu
utambuzi na uteuzi wa kaya masikini alieleza kuwa hufanywa kwa
kushirikisha wananchi wa jamii husika na kumekuwepo na ushirikiano mzuri
baina ya wananchi na maafisa wa mfuko huo.
Chini
ya Mpango huo kaya zinazopata msaada huo ambao zina watoto wenye umri
wa kwenda skuli wanapaswa kuwasimamia kuhudhuria masomo na kwa kaya
zenye wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka 5 wanapaswa
kwenda kliniki kupata matibabu na ushauri wa daktari kama mwongozo wa
afya ya mama na mtoto unavyoelekeza.
Msaada
unaotolewa kwa kaya hizo ni shilingi 34,000 kila baada ya miezi miwili
kwa kaya zenye watoto na wajawazito na shilingi 17,000 kwa kaya
nyingine.
Post a Comment