- Wananchi wa Zanzibar wasema serikali mbili zatosha
- Wachukizwa na wanasiasa wanafiki wanaopindisha pindisha maneno
- Vijana wa CCM kutovumilia wanasiasa wanaokashifu waasisi wa Taifa letu
- Wasema wamechoshwa na matendo ya Viongozi wa Vyama vya Upinzani wataka muswada wa kuujadili Serikali wa Umoja wa kitaifa wataka ufutwe kwani hauna faida kwa maendeleo yao .
Wananchi wakionyesha ishara ya Serikali mbili kwenye mkutano wa CCM kwenye viwanja vya Kibanda Maiti, Unguja Zanzibar.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia kwenye mkutano wa
hadhara wa CCM leo, May 4, 2014, kwenye Viwanja vya Kibandamaiti, mjini
Zanzibar. (Picha na Bashir Nkoromo)
Umati
uliohudhuria kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliohutubiwa na Kinana
leo, May 4, 2014, kwenye Viwanja vya Kibandamaiti, mjini Zanzibar.
Watu wengi wakiwa wamejitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa CCM , May 4, 2014, kwenye Viwanja vya Kibandamaiti, mjini Zanzibar.
Mbili zatosha.
Kila mtu alionyesha mapenzi yake kwa CCM.
Wakazi wa Zanzibar hawakujali mvua iliyokuwa inanyesha kwenye mkutano wa CCM Kibanda Maiti Zanzibar
Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume akihutubia wakazi wa Unguja na kuwaambia kuwa waasisi wetu waliweka uzio wa kutulinda na kudumisha umoja na undugu wetu na kusema uzio huo ni Muungano wetu.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mbunge wa BundaStephen Wassira akihutubia wananchi wa Zanzibar ambapo alisema UKAWA wanatakiwa kuelewa misingi ya Muungano kwanza kisha waje na hoja .
Mbunge wa Songea Mjini Dk Emmanuel Nchimbi akihutubia wakazi wa Unguja kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kibanda Maiti na kuwataka wananchi hao kuwa makini na viongozi wanaogeuza maneno huku akitolea mfano kutoka kwenye kitabu cha Maalim Seif.
Katibu wa NEC Oganizeshen Dk. Mohamed Seif Khatibu akihutubia wakazi wa Unguja kwenye mkutano wa hadhara Kibanda maiti .
Sehemu ya Umati uliohudhuria mkutano wa hadhara ambao ulihutubiwa na Viongozi mbali mbali wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Viongozi wa CCM wakifuatilia kwa makini hoja mbali mbali za kujenga na kuimarisha Muungano.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amekaa pamoja na Makamu wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd (kushoto) Mjumbe wa Kamati Kuu na Mbunge wa Bunda CCM Ndugu Stephen Wassira ,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Borafya Silima (kulia) na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakifuatilia mkutano wa hadhara bila kujali mvua iliyokuwa inanyesha.
Post a Comment