Jose Mara naye alitumbuiza.
MVUA kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo
imetibua shoo ya mkali wa muziki wa Bongo Fleva, Lady Jay Dee
nakusababisha shoo hiyo kusogezwa mbele mpaka itakapotangazwa.
Shoo hiyo iliyopangwa kufanyika katika
ukumbi wa Nyumbani Lounge ambapo mbali na Lady Jay Dee walikuwa
wamealikwa wasanii wengine wakiwemo, Prof. Jay, Patricia Hillary, Roma
mkatoliki, Baghdady na wengine kibao.
Mvua hiyo ambayo ilianza kunyesha toka
majira ya jioni na kuzua hofu ya kuendelea kwa shoo mpaka kufikia saa
saba za usiku mwanadada Jide alipanda jukwaani na kuomba radhi kwa
mashabiki waliokuwa wamehudhuria ukumbini hapo kutokana na hali hiyo
nakuwahaidi kuwa shoo hiyo itarudiwa tena ila kwa wale waliojitokeza
watapatiwa tiketi ya shoo ijayo (Hawatalipa kiingilio tena). Baada ya
kuomba radhi alipiga nyimbo zake kadhaa akifuatiwa na wasanii wengine.
(STORI & PICHA: Andrew Carlos na Deogratius Mongela/GPL)
Post a Comment