Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MBWA ADAIWA KUZAA SUNGURA, PICHA NA TUKIO HUSIKA LIPO HAPAbbbbbbbbbbbbbbbbbbbb




WENYEJI wa kijiji cha Kithenge kutoka wilaya ya Igembe kusini wamebaki vinywa wazi kufuatia tukio la kustaajabisha ambapo mbwa wa jirani yao alijifungua sungura badala ya mbwa wa kawaida.
Kulingana na  mwnenye mbwa huyo Bw Josphat Kairithia, kitendo hiki kilitokea Jumanne wiki iliyopita ambapo alimpata mbwa huyo akimyonyesha na akadhania ni mbwa wa kawaida.
Baada ya kuchunguza zaidi, aligundua kuwa hakuwa mbwa wa kawaida bali sungura na hapo ndipo alianza kuwaita majirani wake waje kumtegulia kitendawili hicho.
Hata hivyo, waliokuja walishtuka zaidi na wengine wakitoroka wakidhania kuwa hayo yalikuwa mazingaombwe.
Kairithia aliongeza kuwa mbwa huyu aliendelea kumnyonyesha sungura huyo kama kawaida na kumpa ulinzi wa mwana.
“Tukio hili limenishangaza sana na siwezi nikaeleza kilichotendeka. Anamnyonyesha sungura huyu kama kawaida na hataki kumuona mtu akimkaribia. wanaokuja kumwona lazima wapitie kwangu ili niweze kumtuliza mbwa huyo la sivyo wakipate cha mtema kuni,” akasema.

Kairithia alitupilia mbali uwezekano kuwa hayo yangekuwa mazingaombwe huku akielezea kuwa  huenda ikawa ni ujumbe kutoka kwa mungu kuwaambia watu wapende maadui wao.

“Siwezi nikasema kuwa haya ni mazingaombwe kwani najua ya kwamba mungu ana njia nyingi za kuongea na watu wake. Labda anataka kutuelezea jinsi ambavyo tunapaswa kuwapenda hata wale ambao tunafikiri ni maadui wetu,” akasema.

Sungura mwingine
Ametupilia mbali fununu za watu ambao wanadai kuwa huenda alimwekea mbwa huyo sungura huyo akisema kuwa hakuwa karibu mambo hayo yakitendeka.

Ili kutoa thibitisho kwa watu, Kairithia alimwekelea sungura mwingine karibu na mbwa huyo na kilichowashangaza wengi ni kuwa hakupoteza muda kumla.

Mamia ya watu wanazidi kutembelea familia hiyo kwa nia ya kuyaona maajbu hayo ya ulimwengu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top