Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Balozi
Seif Ali Iddi akizungumza katika mkutano wa hadhara wa uwanja wa
Demokrasia uliopo Kibanda maiti Mjini Zanzibar.Picha na Hassan Issa wa – Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
---
Msajili
wa Vyama vya Siasa Nchni Tanzania ameombwa kuliangalia kwa umakini
kundi linalojiita Umoja wa Katiba ya Watanzania { UKAWA } lilioamua
kuenesha mikutano ya hadhara inayoashiria mfumo wa kisiasa bila ya
kuzingatia taratibu za kisheria zinazofuata usajili rasmi.
Ombi
hilo limetolewa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya
Chama cha Mapinduzi Balozi Seif Ali Iddi wakati akisalimia kwenye
mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika Uwanja wa Demokrasia Kiband
Maiti Mjini Zanzibar.
Balozi
Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema kundi hilo
lililoundwa na baadhi ya Viongozi wa juu wa vyama vyasKisiasa vya
Upinzani limeshindwa kutekeleza kazi waliyotumwa na Wananchi ya
kutengeneza mfumo wa kupata Katiba mpya kupitia Bunge Maalum la Katiba.
Alisema
kitendo cha Viongozi hao ambacho kinawakosesha wananchi lile
wanalolihitaji kinafaa kiangaliwe kwa umakini na msajili wa vyama vya
siasa kwa vile kinaweza kuwakosesha wananchi hao muda wao wa
kushughulikia mahitaji yao ya Kimaendeleo na kujikita zaidi katika
mikutano hiyo yenye ushawishi zaidi wa kisiasa.
Balozi
vSeif aliwatahadharisha wana CCM na Wananchi wote kujiepusha na kundi
hilo ambalo limekuwa likichukuwa kodi zao bila ya kutekeleza majukumu
waliyo wakabidhi.
“
Kama kweli wana uchungu na nyinyi wananchi mbona walisubiri kwanza
kutia mfukoni mkwanja { posho } halafu ndio wakaingia mitini kuvikimbia
vikao vya Bunge Maalum kwa kujenga hoja “. Alisema Balozi Seif.
Mjumbe
huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM aliwaonya wale
viongozi wa siasa wenye tabia ya kumsakama katika majukwaa ya kisiasa
kuachana na tabia hiyo mara moja kwa vile wengi kati yao anawaelewa
udhaifu wao wa Kisiasa.
Alisema endapo kama viongoz hao wataendelea na hulka hiyo waelewe kwamba muda si mrefu atalazimika kufichua maovu na aibu zao.
Post a Comment