MSHAMBULIAJI
wa zamani wa kimataifa wa England, Michael Owen anaamini Cristiano
Ronaldo ndiye mchezaji mkubwa zaidi kwa wakati wote katika klabu ya Real
Madrid.
Ronaldo
amekuwa katika kasi kubwa msimu huu na kuvunja rekodi ya kufunga mabao
mengi zaidi katika msimu mmoja wa UEFA baada ya kupiga mawili katika
ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Bayern Munich katikati ya wiki hii na
kufikisha magoli 16.
Owen
aliyeichezea Real Madrid msimu wa 2004-05 amevutiwa na kiwango cha
Ronaldo na kuthubutu kusema kwasasa nyota huyo ni tunu ya klabu zaidi ya
Ferenc Puskas.
“Nadhani
mchezaji mkubwa zaidi kwa wakati wote Real Madrid ni Cristiano Ronaldo
akifuatiwa na Ferenc Puskas”. Owen ameandika katika kolamu yake kwenye
gazeti la Sportlobster .
“Ronaldo amelingana na Puskas” . amekuwa na rekodi kubwa ya mabao 242 katika mechi chache.
“Pia
amekuwa mchezaji wa kwanza wa Real Madrid kufunga mabao 100 kwa haraka
zaidi na ameshikilia rekodi ya kuifungia Madrid mabao mengi zaidi ndani
ya msimu mmoja”.
Pia
kwa kifupi, Owen alielezea maisha yake alipokuwa Real Madrid kuwa
yalikuwa mazuri kwa kazi yake hasa kwa vyombo va habari na mashabiki
wake.
Michael Owen enzi zake akiwa Real Madrid |
“Sikuwa na wasiwasi ya kutopata mafanikio katika uwanja maarufu.
“Nilikuwa
na mambo mawili: Nitafanya nini nitakaposhika mpira kwenye utambulisho
wangu Santiago Bernabeu na pili nitakaa wapi katika vyumba vya
kubadilishia nguo”.
“Nilikuwa katika wasiwasi mkubwa wakati wa utambulisho”.
“ Nilikuwa nafirikia maujanja ya kufanya nitakapotupiwa mpira.
“Nilionesha ufundi mkubwa mbele ya vyombo vya habari na mashabiki waliokuwepo Bernabeu”.
“Hakukuwa na jinsi ya kushindwa mbele ya vyombo vya habari vya dunia”.
Ghafla Owen aliondoka Madrid ndani ya msimu mmoja akifunga mabao 14 tu katika mechi 36 za La Laiga alizocheza.
Post a Comment