Aprili 6, mwaka huu ni siku ambayo mkazi wa Kijiji cha Kibanda wilayani Kyela, Mboka Mwakikagile (20) haitaisahau.
Ni siku ambayo aliibiwa mtoto mchanga wa kiume aliyekuwa na umri wa siku saba tu.
Akisimulia
tukio hilo, Mboka anasema alijifungua salama Machi 30 akiwa nyumbani
kwa wazazi wake ambao ni Lupalo Mwakikagile (90) na mkewe Nelly Kyusa
(49).
Anasema
akiwa katika siku ya saba, alipigiwa simu na mzazi mwenzake (jina
linahifadhiwa) kwamba mama yake mkubwa atafika nyumbani kumwona mtoto.
Anasema baada
muda mfupi mwanamke huyo alifika kwa pikipiki akiwa na mkoba uliokuwa
na nguo za mtoto, sabuni na vifaa vingine. "Baada ya kumkaribisha na
kusalimiana na wote , mwanamke huyo alimchukua mtoto na baadaye
alinishauri twende Zahanati ya Njisi akatibiwe jicho ambalo lilikuwa
linamsumbua kidogo,''anasema.
Mboka na
mwanamke huyo waliondoka kwenda kwenye zahanati hiyo kwa pikipiki na
kwamba baada ya kufika hapo, daktari aliwataka wanunue daftari na
mwanamke huyo alitoa Sh2,000 na kumtaka akanunue.
''Nilipokea
fedha hizo na kumwachia mtoto pamoja na simu yangu wakati mimi
nikielekea kununua daftari kwenye duka lililo mbali na zahanati hiyo,''
anasema.
Anasema
mara baada ya kurudi dukani alishtuka kutomwona mwanamke na mtoto
wake.'Kitendo hicho kilinishtua zaidi kwani mzazi mwenzangu aliondoka
bila ya kunishirikisha kwamba tukaripoti polisi na kibaya zaidi yeye
ndiye aliyedai kwamba ni mama yake mkubwa,'' anasema
CHANZO MWANANCHI
Post a Comment