Na Woinde Shizza,Arusha.
Jaji mstaafu Mark Bomani jana (leo )amezindua rasmi video ya wimbo
wa waandishi wa habari ujulikanayo kwa jina la Uhuru wangu pamoja na
albamu mpya ya msanii wa mziki wa nyimbo za asili Mrisho Mpoto
ijulikanayo kwa jina la Waite katika kilele cha maathimisho ya uhuru
wa vyombo vya habari duniani.
Uhuru wangu uko wapi mwanahabari mie,kalamu yangu,sauti yangu kamera yangu leo ndio kaburi langu mie.Huo ndio wimbo wa kundi la Mrisho Mpoto Band ambalo ulikuwa ukiwaburudisha wanahabari katika uzinduzi wa albamu Mrisho Mpoto Band,unaoelezea mambo mbalimbali wanayokumbana nayo wanahabari wa vyombo mbalimbali vya habari.
Akighani mashairi ya wimbo huo katika uzinduzialisema poleni sana misa
Tanzania,TMF,MOAT,UTPC ,TCRA kama mtu ile timu ya watu watano
tuyioituma Ujerumani ,Norway,Sweden ipo wapi ripoti yake
Akiongea wakati wa uzinduzi wa albamu hiyo pamoja na wimbo huo wa
wanahabari msanii mrisho mpoto alisema kuwa yeye alifarijika sana pale
alivyofatwa na wanahabari na kumuomba awatungie wimbo ambao
unawahusu wanahabari pamoja mambo ambayo yanawakabili.
Alisema kuwa wamekaa wakashauriana na timu yake na bendi yake kuwa watu wasanii wengi wamekuwa wakizindua albamu kwa kuweka viingilio vikubwa kualika watu wengi lakini yeye binafsi ameamua kuzindua albamu hii katika siku hii ya waandishi wa habari kwa kuwa wamemtoa mbali na anakitu cha kuwapa zaidi ya kuwapa zawadi hii ya kuzindua albamu yake mbele yao.
Alibainisha kuwa mbali nakuzindua albamu hiyo pia kwa kuwa waandishi wamempa hadhi ya kuwatungia wimbo pia anajitolea kuweka wimbo huu wa waandishi wa habari ndani ya albamu yake ili kila mtanzania na mshabiki wake ambaye atanunua albamu yake aukute wimbo ndani ya albamu yake.
"Hii albamu yangu itakuwa na nyimbo zangu zote ikiwa na wimbo wa
nikipata nauli adi nyimbo zake zote ambazo zinajulikana na kiukweli
najisikia kulia sana kupewa heshima hii nzito ya kuzindua albamu yangu
na ata jana nilivyokuwa nakuja uku nilikuwa na zunguma na mh bomani
kuwa hii kwangu itakuwa ni historia katika maisha yake"alisema mpoto
Katika wakati wimbo huu ukiendelea wanahabari walionekana wakitoa
machozi kwa kuuzunishwa na tenzi zilizopo katika wimbo huu kwani
msanii huu ameuimba kiualisiazaidi.
Post a Comment