Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Colombia waanza vizuri kombe la dunia kwa kuilaza Ugiriki 3-0

 
Goli la mapema lililofungwa na mlinzi Pablo Armero katika dakika ya tano ya mchezo, kisha mshambuliaji Abel Aguilar Gutierez katika dakika ya 58 akifunga kwa mguu wa kushoto katika dakika ya 58 na lile la mwisho lililofungwa na kiungo James Rodriguez yaliifanya timu hiyo ya Amerika Kusini kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Ugiriki iliyoanza na wachezaji kumi wa klabu ya Olympiacos .
Colombia waliokuwa na safu imara ya ulinzi wamejiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu kwa hatua ya 16 kutoka kundi C.

Ikicheza soka la kushambulia na mchezo wa nguvu, Colombia iliwazidi kwa muda mwingi Ugiriki na mabingwa hao wa zamani wa Ulaya waliishia kugongesha nguzo mara moja katika mchezo ambao hawakufanya mashambulizi ya kutosha.
Ilikuwa ni mechi yenye faulo nyingi, Colombia walicheza faulo 19 wakati Ugiriki walifanya faulo mara 14.
Viungo wa Ugiriki, Kostas Katsouranis, Panagiotis Kone, Loannis Maniatis, Giorgos Samarasna Dimitris Salpigidis walitawala mchezo lakini walishindwa kutengeneza nafasi za kufunga kwa mshambulizi pekee, Theofanis Gekas.
Walitengeneza nafasi mbili tu za hatari na hawakufunga goli lolote wakati wapinzani wao Colombia walitengeneza nafasi sita na kufunga magoli matatu japokuwa Ugiriki ilionekana kumiliki mpira kwa asilimia 52 dhidi ya 48 za Colombia.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top