Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HIVI NDIVYO BAROTELI ALIVYOPELEKA KILIO ENGLAND, HUKU IVORY NI CHEREKOCHEREKO KWA KUIBANJIA JAPAN


Mabingwa wa zamani wa kombe la dunia Italy imeanza vyema kampeni yake ya kuwania kombe la dunia nchini Brazil baada ya kuichapa Uingereza mabao mawili kwa moja katika mechi kali. 
 Didier Drugba na Gervinho wakishangilia bao lao
Ivory Coast ilijipatia mabao yake kupitia wachezaji Wilfried Bony na aliyekuwa mchezaji wa Arsenal Gervinho (pichani) huku Japan ikifunga kupitia mshambuliaji wake keisuke Honda.
Bao la ushindi la Italy lilifungwa kwa kichwa kupitia mshambuliaji matata Mario Baloteli mda mchache tu baada ya kipindi cha mapumziko. Awali mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge alikuwa amekomboa bao lililofungwa na Claudio Marchisio wa Italy.
Mechi hiyo ilichezwa chini ya viwango vya juu vya joto katika uwanja wa Manaus uliopo katikati ya msitu wa Amazon.Katika mechi za awali ,Costa Rica ilitoka nyuma na kuishinda Uruguay mabao matatu kwa moja huku Colombia nayo ikiicharaza Ugiriki mabao matatu bila katika mji wa Belo Horizonte.
Wakati huohuo miamba ya soka barani Afrika Ivory Coast imeimarisha matumaini ya bara hili baada ya kutoka nyuma na kuishinda Japan kwa mabao 2-1.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top