Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipokewa na wenyeji wake wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa
Bolivia juzi Juni 13, 2014 kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka
50 ya Nchi za G 77 na China, yanayofanyika leo Juni 15, 2014, jijini
Santa Cruz, Bolivia.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Meya wa Jiji la Santa Cruz, Percy Fernandez, wakati
alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Bolivia juzi Juni 13, 2014
kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya Nchi za G 77 na
China, yanayofanyika leo Juni 15, 2014, jijini Santa Cruz, Bolivia.
Kushoto ni Mama Zakhia Bilal.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika mazungumzo na Rais wa Bolivia, Evo Morales, walipokutana
kabla ya kuhudhuria maadhimisho ya Miaka 50 ya nchi za G77 na China
yanayofanyika jijini Santa Cruz, Bolivia, jana Juni 14, 2014. Katikati
ni Mkalimani wa Rais wa Bolivia. Katika mazungumzo hayo Rais Morales
aliishukuru Tanzania kushiriki katika maadhimisho haya na akasisitiza
kuwa uhusiano wa nchi za G77 unapaswa kuenziwa huku Mheshimiwa Makamu wa
Rais Dkt. Bilal akifafanua kuwa Tanzania inatambua na kuheshimu
jitihada zinazofanywa na umoja huo na kwamba ni kipindi kizuri
kuadhimisha miaka 50 kwa kutafakari kuhusu kutanua fursa za kukuza
uchumi ili kuendeleza wananchi wa nchi hizo.

akiongozana na mwenyeji wake Rais wa Bolivia, Evo Morales, baada ya
mazungumzo yao yalioyofanyika jijini Santa Cruz, Bolivia, jana Juni 14,
2014.
Makamu
wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
akiagana na Mwenyeji wake Rais Evo Morales, Rais wa Bolivia baada ya
kufanya mazungumzo saa chache kabla ya kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka
50 ya nchi za G77 na China yanayofanyika jijini Santa Cruz, Bolivia.
Katika mazungumzo hayo Rais Morales aliishukuru Tanzania kushiriki
katika maadhimisho haya na akasisitiza kuwa uhusiano wa nchi za G77
unapaswa kuenziwa huku Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal akifafanua
kuwa Tanzania ni inatambua na kuheshimu jitihada zinazofanywa na umoja
huo na kwamba ni kipindi kizuri kuadhimisha miaka 50 kwa kutafakari
kuhusu kutanua fursa za kukuza uchumi ili kuendeleza wananchi wa nchi
hizo.
Post a Comment