Mfanyabiashara
wa madini, Richard Lucas (29) anadaiwa kujiua kwa kujipiga risasi
kichwani baada ya kusababisha ajali mbili tofauti. Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema alijipiga risasi juzi saa 12:45
jioni nyumbani kwake eneo la Kimandolu. Alitumia bastola aina ya Luger
yenye namba B136986 . Alisema uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kuwa
Lucas alitokea Tengeru akiwa na gari aina ya Toyota Rav 4 yenye namba
za usajili T 494 CKY alikokuwa amemfuata rafiki yake aliyekuwa amepata
ajali ya kugongwa na gari.
Baada ya hapo gari ya Lucas ilipinduka na waliokolewa kwa kupitia dirishani na wananchi.
Inadaiwa
alitoka eneo la tukio kwa pikipiki ya kukodi kwenda nyumbani kwao
Kimandolu huku akimwacha Vick Mchuma kwenye eneo la tukio.
Alisema
baada ya muda, Mchuma ambaye waliongozana naye kwenda kumsaidia rafiki
yao aliyepata ajali Tengeru, alipata taarifa kuwa Lucas amejipiga risasi
na mwili upo Hospitali ya Mount Meru. Polisi wanaendelea na uchunguzi
wa tukio hilo.


Post a Comment