Kulia ni Mganga chasama akitibu mtoto aliyekuwa amevunjika mguu kuanzia pajani mtoto huyo alishapona,kushoto ni mama wa mtoto na katikati ni bibi wa mtoto |
Mganga Chasama kulia akiwa katika picha ya pamoja na mgonjwa aliyevaa jezi kiatikati baada ya kumtibu na kupona |
kulia ni Mganga chasama akiwa na mgonjwa aliyewahi kumtibu mguu uliovunjikia kwenye kiwiko-Picha zote na Victor Bariety wa malunde1 blog-Geita. |
TIBA za asili zilianza kutumika tangu
enzi za mababu zetu, lakini zilikuja kupoteza umaarufu wake baada ya
kuingia kwa wakoloni walioleta dawa.
Pamoja na matumizi ya dawa asili
kupungua baada ya ujio wa wakoloni, siku za karibuni muamko wa
Watanzania kurudi katika dawa hizo umeanza kuongezeka huku ikielezwa
kwamba imechangiwa na madhara wanayoyapata watu wanapotumia baadhi ya
dawa za hospitali.
Hivi karibuni, mmoja wa matabibu wa tiba
hizo za asili,Paul Chasama Luswigilo (52), alifanya mahojiano na
mwandishi wa malunde1 blog Victor Bariety na kuzungumzia jinsi
anavyowasaidia watu mbalimbali akitumia utaalamu huo aliorithi kwa
marehemu baba yake Chasama Luswigilo.
Tofauti na matabibu wengine, Chasama
anasema amejikita zaidi kutoa tiba za mifupa ambapo huwa anatumia picha
zinazopigwa hospitali (x-ray) kabla hajamtibu mgonjwa.
Miongoni mwa wagonjwa ambao amekuwa
akiwahudumia kwa wingi ni waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda ambao
hujeruhiwa wakiwa kazini.
Majeruhi hao wa pikipiki wamekuwa
wakiongezeka kila kukicha na kufikia hata kupoteza maisha tangu usafiri
huo uliporuhusiwa na serikali kutumika.
“Kwa kweli huwa nikienda pale
wodini katika hospitali ya Wilaya ya Geita,na kukuta wagonjwa
wakigalagala na kusikilizia maumivu nasikitika sana’’
“Hii yote ni kwa kuwa wanadhani
tiba inapatikana tu hospitali bila kujua kuna wataalamu kama sisi
tunaoweza kuwaondolea maumivu hayo, tena kwa wepesi,” anasema.
Katika dawa zake hizo kwa wale waliopata
ajali na majeraha yao kuonekana kuvilia damu, huwa na dawa maalumu
ambayo humwekea mgonjwa na kuyeyusha damu hiyo.
Wakati kwa upande wa wagonjwa
waliowekewa vyuma, kuna dawa ya kupaka ambayo husaidia kupunguza maumivu
na uvimbe unaokuwepo kati ya chuma na ngozi.
Anasema kwa wajawazito ambao wamekuwa
wakifanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua, ana dawa yao ya kuwaepusha
kuwa na kovu kubwa la mshono pindi wanapopona na ya kuwaondolea maumivu
ya mgongo na kiuno yanayowatokea mara kwa mara.
Tatizo jingine analotibu mtabibu huyu ni
la watoto kushindwa kukaza shingo, hasa wanapofikia hatua ya kukaa na
wale waliozaliwa na ulemavu wa viungo ambao anasema kutokana na mifupa
yao bado kuwa michanga ni rahisi kuwatibu.
Wakati akiwa na tiba hizo, Chasama
anaumia sana kuona kwamba haziwezi kutumika hospitali kama tiba mbadala
kwani anapofika maeneo hayo anatamani awaambie madaktari, lakini
kutokana na sheria za kitabibu inashindikana.
Kutokana na hali hiyo alitaka kuwepo na
utaratibu wa kubadilishana wagonjwa kati ya watabibu wa tiba asili na
hospitali, anaosema umefanikiwa kwa kiasi kikubwa nchini China.
Katika harakati za kufikia huko, anasema
anao mpango wa kupeleka dawa zake kwa mkemia mkuu ili kwenda
kuthibitishwa ubora wake, na pia ana mpango wa kuzungumza na Hospitali
mbalimbali zenye vitengo vya viungo ili kutumia dawa zake ikiwemo ile
ya kuweka ndani ya P.O.P na kumsaidia mgonjwa kubaki na maumbile yake
kwani wengine hujikuta wakivimba au wakibadilika rangi eneo wanalofungwa
bendeji hiyo ngumu.
Chasama amekuwa na changamoto mbalimbali
anazokabiliana nazo katika kufanya kazi zake ikiwemo ukosefu wa mashine
ya kumwezesha kusaga dawa hadi kufikia hatua ya poda kwa madai kwamba
nazo ni ngumu kutengeneza kama ilivyo mifupa.
Anasema mashine hiyo inatumia nguvu za
umeme zenye watt 1000, wakati kwa sasa kutokana na kutokuwa na uwezo
anatumia kifaa aina ya blender na kutwanga kwa kutumia kinu kisha
kupitisha kwenye chekecheo.
Wito wake kwa jamii ni kuwa na imani na
dawa zao, kwa kuwa wengi wao mbali na kutomaliza dozi kama
wanavyotakiwa, wamekuwa wa kwanza kuuliza kama kweli watapona, maswali
ambayo anadai si rahisi kuulizwa daktari wa hospitali.
Pia amewataka kuhakikisaha wanayalinda
mazingira ili kuweza kuhifadhi dawa za asili ambazo nyingi zinapatikana
katika misitu ya asili.
Anaitaka serikali kujenga utaratibu wa
kubadilishana wagonjwa kwa kuwa magonjwa mengine hayatibiki hospitali,
huku akitolea mfano kwamba huwa anapata wagonjwa madaktari ofisini
kwake.
Kuhusu kiwango chake cha elimu, anasema
mbali na elimu yake ya msingi aliyonayo,marehemu baba yake alimfundisha
masuala ya huduma ya kwanza, hivyo anajua vema kumhudumia mgonjwa
atakayefika kwake akiwa mahututi.
Chasama anasema amekuwa akitoa huduma
hata kwa wakazi wa mikoani bila hata ya kuja kwani zaidi atahitaji picha
zao na kama ni dawa anawatumia kwa njia yoyote ambayo itakuwa rahisi
kwao.
JAMHURI lilifanya mahojiano na baadhi ya
wagonjwa waliotibiwa na Chasama , akiwemo Mwesi anayedai alivunjika
mguu baada ya kupata ajali ya gari alipokuwa kwenye kazi yake ya utingo
akitokea Kahama kuja Geita.
Anasema ilikuwa mwaka 2010 alipopatwa na ajali hiyo, lakini baada ya kwenda hospitali alielezwa anapaswa kukatwa mguu wake.
Kutokana na hali hiyo aliwaeleza ndugu zake watafute njia mbadala ya kunusuru mguu wake huo usikatwe.
Anasema wakati akiwa katika kujiuguza
huko ndipo alipompata ndugu yake mmoja aliyewahi kutumia dawa za
Chasama, ambaye alimpeleka na tangu alipotumia dawa hizo ndani ya mwezi
mmoja alipona mguu wake ambao uliunga kabisa na anaendelea na kazi zake
za utingo kana kwamba hakuwahi kupata ajali na kuvunjika mguu.
Mgonjwa mwingine aliyejitambulisha kwa
jina la Rameck anasema alipata ajali mwanzoni mwa mwaka 2013 akiwa
kwenye machimbo ya dhahabu huko Nyarugusu na kuvunjika mguu kwenye
viwiko. Alikwenda hospitali na kufungwa P.O.P, lakini bado mguu huo
ukaendelea kumuuma.
Anasema alipofika kwa Chasama baada ya
kupelekwa na rafiki yake, alipatiwa tiba na hadi sasa alikwisha sahau
kama amewahi kuvunjika mguu.
Wengi wanaweza kujiuliza huyu tabibu ni
nani?Paul Chasama Lushwigilo si geni masikioni mwa watu wengi ndani na
nje ya nchi hususani wale wanaofuatilia vyombo vya habari,hususani
magazeti na mitandao ya kijamii.
Jina lake limeanza kuvuma hivi
karibuni kwenye vyombo vya habari mara baada ya kumpokea na kuanza
kumtibu mgonjwa aliyepooza mwili wake kuanzia kifuani hadi miguuni na
kuoza makalio yake kisha kutimuliwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando
alikokuwa amelazwa baada ya kupata ajali hivi karibuni.
Mgonjwa huyo,Joseph Luhogola(38),mkazi
wa kitongoji cha Nyabugera,Kijiji cha Mganza Wilayani chato katika Mkoa
wa Geita,alipokelewa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Aprili 22
mwaka huu akitokea katika hospitali ya Wilaya ya Chato muda mfupi baada
ya kupata ajali na alitimliwa hospitalini hapo Mei 27 mwaka huu.
Haijajulikana hadi sasa kisa cha wauguzi
na madaktari wa Bugando kumtimua mgonjwa huyo katika hali hiyo ambayo
hata hivyo ilitokana na uzembe wao wenyewe.
Alipotafutwa Mkurugenzi wa Hospitali
hiyo Dk Charles Majinge naye hakuwa na majibu ya kuridhisha ambapo
alisema hajui kama hicho kidonda kilisababishwa na ajali au la,na
kueleza kwamba inawezekana kule kulala kwa muda mrefu kutokana na
kupooza huko alitengeneza kidonda.
“Ili kuweza kueleza haya Mgonjwa aje
Tuone,Tutafute jarada lake tuweze..kufuatilia ni nini kilitokea na sio
kawaida mtu kumruhusu akiwa na kidonda kikubwa kama unavyokielezea,”alisema majinge na kuongeza.
“Labda walimweleza mgonjwa
hawakuwaeleza ndugu na ndiyo maana hawakujua kama ana hali hiyo,sasa
mwambie aje na nyaraka za Taarifa zake.Lakini kuna tatizo la watu kama
hao wamekuwa wakiomba ruhusa ya kuagwa ili waende kwa waganga wa
kienyeji hasa hao wenye kupooza mwili’’.
Alifafanua kwamba”Siwezi kusema kama
hakuna kidonda na kwa tatizo hilo kulingana na Vitanda vyetu,Tatizo la
kuendeleza kidonda lipo,Na wengi wanaokuja hapa wanaomba kuruhusiwa ili
kwenda kwa waganga wa kienyeji”
Wakati Dk Majinge anadai hivyo,mgonjwa
Luhogola(38),anadai alifikishwa Bugando akiwa na majeraha sehemu za
kichwani na yalipona kwa muda mfupi,na kwamba matatizo mengine kama
kupooza na kuoza makalio hakuwahi kuwa nayo na kwamba kauli yake
inalenga kujitetea mbele ya wakubwa zake na kwa watanzania ambao
wameguswa na ugonjwa wake.
Hata hivyo baadhi ya watu walioguswa
na kituko hicho,mbali na kusikitishwa na tukio hilo wao walimtaka
mwandishi wa habari hizi kutoa mawasiliano ya Mtaalamu wa tiba za asili
upande wa mifupa aliyejitoa mhanga kuokoa maisha ya kijana Luhogola
almaarufu Mtoto wa Bugando.
Lengo la wasomaji si jingine bali
walidai tukio hilo limewashitua sana hivyo na kwamba kuna wagonjwa wengi
ambao wanasumbuliwa na matatizo kama hao na wamekuwa wakifia
mahospitalini kwa kukosa msaada wa wataalamu na kwamba iwapo namba zake
zikiwekwa wazi yawezekana ataokoa roho za watanzania wengi.
Huyu ndiye Paul Chasama
Paul Chasama,alizaliwa 1962 katika kitongoji cha Bulima,Kijiji cha Nyabusalu Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza.
Chasama ambaye ni mtaalamu wa tiba za
jadi kwa kuunga mifupa na kurudisha viungo vya mwili vilivyochengana
alianza kutibu mifupa iliyovunjika na watu waliopooza mwili Tangu mwaka
1997 alipoanza kutoa tiba hiyo na kwamba utalaamu huo aliupata kutoka
kwa wazazi wake.
Wakati Chasama anaanza kazi hiyo alikuwa katika kijiji cha Nyarugusu Wilayani Geita Mkoani Mwanza.
Akimzungumzia Mgonjwa huyo,Chasama
anatamba kuwa anao uhakika wa kupona ugonjwa unaomsumbua(wa kupooza) na
kwamba watanzania wakae mkao wa kula kumuona mwenzao akiwa anadunda
mtaani kwani tatizo kubwa ni kidonda ambacho alidai nacho kitatoweka na
kubaki historia.
Anasema“Walichokosea huko Hospitalini
ni kule kumlaza chali kila siku bila kumgeuza hali iliyosababisha kuwa
na kidonda kama hicho.Lakini suala la Kupooza halitachukua Muda mrefu na
hata hiki kidonda kitayeyuka na watanzania hawataamini kitakachotokea”
Nakwambia hivi ndugu mwandishi,mimi
ndiye Chasama kama umewahi kumsikia ninachokueleza ndugu mwandishi huyu
mgonjwa nitamponya na kama kuna mtu haamini asubili aone,nimeshakutana
na kesi kubwa na huyu hapa naweza kusema haumwi lakini niliwaponya na
sasa ukiwaona huwezi amini kama waliwahi kuumwa.
AINA YA WAGONJWA ANAOWAPOKEA
Anasema amekuwa akipata wagonjwa wenye
matatizo kama hayo pamoja na wale waliovunjika mifupa,kuhama viungo na
kuvunjika miguu lakini wamekuwa wakipona kwa kutumia miti shamba.
Hata hivyo alifichua siri kubwa baada ya
kudai kubwa asilimia kubwa ya wagonjwa anaowapokea ni wale ambao tiba
za hospitalini zinakuwa zimeshindwa kufanya kazi.
Aliwataka watu wenye wagonjwa
wanaosumbuliwa na uti wa mgongo,viungo vya mwili vilivyochengana,vidonda
vya tumbo na kupooza wafike haraka katika kitongoji cha Mwenge,Kijiji
cha Nyankumbu Wilayani Geita ili wapate huduma hizo.
Alidai kuwa,kumekuwepo na desturi kwenye
baadhi ya hospitali zetu za kuwakata miguu watu wanaopata ajali za
magari na pikipiki jambo alilodai hawatendewi haki na kuwaomba wenye
matatizo kama hayo kufika mara moja ofisini kwake Nyankumbu Geita.
‘’Kuna watu wamekuwa wakipata ajali na
kuvunjika miguu,na wanapofikishwa hospitalini miguu hiyo humaliziwa kwa
kukatwa,hii siyo halali hata kidogo na mimi nipo kwa ajili ya kazi ya
kuponya watun kama hao,hata kama kuna mtu aliyesagwa mifupa yake ikawa
unga mimi ninao uwezo wa kuirejesha katika hali yake ya awali.
Chasama amesema iwapo atapatiwa msaada
na wasamalia wema atatimiza malengo yake kwa kufungua CLINIC kubwa ya
kutibu magonjwa yote ambayo anao utaalamu wake.
Aidha Chasama aliiomba serikali
kuwathamini wataaalamu kama na ikibidi iangalie uwezekano wa kuwachukua
wataalamu wote wanaorudisha viungo vya mwili vilivyochengana na kuwaweka
kwenye hospitali zetu ili wasaidiane na madaktari kuokoa roho za
watanzania.
WALIOTIBIWA NA CHASAMA WANENA
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi
baadhi ya watu ambao walikuwa na matatizo kama ya Luhogola na sasa
walikwishapona,waliwataka watanzania wenye matatizo kama hao kukimbilia
kwa Chasama kuokoa roho zao.
Walisema,Chasama anastahili pongezi kwa
kile walichodai mbali na kuwa na tiba za uhakika hatozi kiwango kikubwa
cha pesa na anachojali ni utu.
‘’Huyu Chasama ni wa kupongezwa maana
kama unatatizo hakimbilii pesa yako bali anakutibu na ukishapona ndiyo
anakuchaji pesa kidogo tofauti na waganga wengine’’alisema Mwesi
aliyewahi kuvunjika paja baada ya kupata ajali na aliyemponya ni
Chasama.
Bw,Mayengo Mayengo,aliyewahi kuwa na
tatizo la kuhama kwa nyonga,Rameck Rameck aliyevunjika mguu sehemu ya
kiwiko wamedai kuwa hakika bila Chasama hawajui kwa sasa hali zao
kimaisha zingekuwaje na wanamshukuru kwa kuwaponya maana mpaka sasa
wanaendelea kupiga mzigo na kujiingizia kipato.
Baadhi
ya mawasiliano ya simu ya watu ambao wamewahi kutibiwa na kupona ni
pamoja na Mama Shabani 0686739829,Rameck 0789937517,Mayengo
0756822690,na Eliud 0785418686 iwapo huamini unaweza kuuliza kwa hawa
ambao wamewahi kunufaika na huduma ya Chasama.
KAMA KUNA MTU ANA TATIZO AWASILIANE NA MTAALAMU WA KUUNGA MIFUPA CHASAMA KWA SIMU 0787469670
Na Victor Bariety-Malunde1 blog Geita
Post a Comment