Balozi wa Marekani hapa nchini Bw. Mark
Childress (kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa
Helkopta kutoka kwa Taasisi ya Howard G. Foundation inayomilikiwa na
mfanyabiashara mashuhuri nchini Marekani Bw. Warren Buffet (hayupo
pichani) kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyarandu.Hafla
hiyo imefanyika jana jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Idd Mfunda (kushoto)
na Afisa Mtendaji Mkuu & Rubani Mkuu wa Kampuni ya Helkopta Charter
(EA) Ltd Bw. Peter Achammer wakitiliana saini katika hati za
makabidhiano ya Helkopta moja iliyotolewa kama msaada na Taasisi ya
Howard G. Buffet Foundation ya nchini Marekani.Wanaoshuhudia zoezi hilo
ni Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyarandu (aliyesimama kushoto)
na Balozi wa Marekani hapa nchini Mark Childress
Waziri
wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akionyesha ufunguo wa Helkopta
mara baada ya kukabidhiwa na Afisa Mtendaji Mkuu & Rubani Mkuu wa
Kampuni ya Helcopter Charter (EA), Peter Achammer kwa niaba ya Mfuko wa
Howard G. Buffet ambapo ni moja ya utekelezaji wa ahadi za mmiliki wa
Mfuko huo alizozitoka kwa Rais Jakaya Kikwete alipofanya ziara katika
Mbuga za wanyama hapa nchini hivi karibuni.Wa pili kulia ni Balozi wa
Marekani nchini, Mark Childress naWaziri Kivuli wa Maliasili na Utalii,
Mchungaji Peter Msigwa .
Waziri
wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akiwa amepanda Helkopta ambayo
alikabidhiwa kama msaada kutoka Mfuko wa Howard G. Buffet kwa ajili ya
kusaidia juhudi za Serikali katika kupambana na ujangili.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akiteta jambo na Wawakilishi wa
Bunge .katika hafla ya makabidhiano ya msaada wa Helkopta kwa ajili
kupambana na ujangili nchini Mh. James Lembeli ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Maliasili na Mazingira (katikati) na Mhe.
Mch. Peter Msigwa Waziri Kivuli wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Meneja
Mipango na Mikakati wa Howard G. Buffet Foundation Tanzania Chapter Bi.
Ellen Mutalemwa akitoa rai wakati wa hafla ya kukabidhi Helkopta moja
ambayo ni kati ya ahadi zilizotolewa na Mwenyekiti wa Mfuko huo
alipomtembelea Rais Kikwete hivi karibuni. Helkopta hiyo imetolewa ili
kusaidi juhudi za Serikali katika kupambana na ujangali katika hifadhi
za Taifa.
Post a Comment