Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WITO WADAU KUTOA MAONI YA MISWADA YA SHERIA YA: VALUE ADDED TAX ACT, 2014, TAX ADMINISTRATION ACT, 2014 NA FINANCE ACT, 2014

 

A48CFF38-06EC-4219-B711-37821DA45A9F_mw1024_n_sJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA
WADAU KUTOA MAONI YA MISWADA YA SHERIA YA: VALUE ADDED TAX ACT, 2014, TAXADMINISTRATION ACT, 2014 NA FINANCE ACT, 2014
_____________
Katibu wa Bunge anawatangazia wananchi wote kwamba Kamati ya Bunge ya Bajeti itaanza kuchambua Miswada ya Sheria ya: Value Added Tax Act, 2014, Tax Administration Act, 2014 na Finance Act, 2014 siku ya Jumanne tarehe 17 Juni, 2014 kwa lengo la kuuboresha kabla ya kupelekwa Bungeni kusomwa mara ya pili na hatimaye kutungwa kuwa Sheria.
 Kwa mujibu wa Kanuni ya 84(2) ya Kanuni za kudumu za Bunge, Toleo la April, 2013 Kamati ya Bunge iliyopelekewa Muswada na Mheshimiwa Spika inaweza kumwalika mtu yeyote au taasisi yoyote kwa njia ya matangazo au kwa kuwaandikia barua ya mwaliko kufika mbele ya Kamati na kutoa maoni yao.Hivyo basi, Kamati ya Bajeti inakaribisha wadau wenye maoni ya kuboresha miswada ya Value Added Tax Act, 2014, Tax Administration Act, 2014 kuwasilisha maoni hayo kwa Maandishi kwa Katibu wa Bunge, Ofisi ya Bunge, S.L.P 941, Dodoma. Kikao cha kusikiliza na kupokea maoni hayo kitafanyika  siku ya Jumanne tarehe 17 na Jumatano tarehe 18 Juni, 2014.

 Maoni kwa ajili ya Finance Act yatapokelewa na kusikilizwa siku ya Alhamisi tarehe 19 na Ijumaa tarehe 20 Juni, 2014. Aidha, Kamati inapendekeza kuwa maoni yawasilishwe kupitia makundi ama asasi zenye maslahi yanayofanana ili yaweze kushughulikiwa kwa pamoja.
 Maoni kuhusu Miswada hiyo, yatasikilizwa katika tarehe tajwa kuanzia saa 5.00 asubuhi, Ukumbi wa Msekwa uliopo Bungeni Dodoma. Aidha, maoni hayo yanaweza kutumwa kwa njia ya barua pepe kwa anuani lkitosi@parliament.go.tz. Kwa ufafanuzi zaidi wasiliana na Sekretarieti ya Kamati kupitia nambari +255716909526, +255785570685 au +255756160006.
 Miswada hiyo inapatikana katika Tovuti ya Bunge www.parliament.go.tz.
 Imetolewa na:
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa
Ofisi ya Bunge
DODOMA
14 Juni 2014
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top