Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

AJALI MBAYA YA FUSO YAUA NA KUJERUHI SHINYANGA

UMATI WA WAKAZI WA KIJIJI CHA UCHUNGA WAKITAZAMA AJALI YA FUSO
Miili ya marehemu ikiwa katika eneo la dharura katika hospitali ya mkoa wa shinyanga

Hapa ni katika eneo la dharura katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga ambapo majeruhi 29 hadi sasa wamepokelewa kufuatia ajali ya gari aina ya fuso iliyokuwa imebeba watu wengi pamoja na mizigo kuelekea katika mnada wa Mhunze uliopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.Ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo Alhamis.Pichani majeruhi waliendelea kuhudumiwa na wataalam wa afya katika hospotali ya mkoa wa Shinyanga

Kwa mujibu wa kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel ameiambia malunde1 blog kuwa mpaka sasa wamepokea miili miwili ya marehemu na majeruhi 29
Huduma inaendelea kutolewa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga


Baadhi ya majeruhi wameiambia blog Hii kuwa gari aina ya fuso waliyokuwa wamepanda tena kwa kujazana ilikuwa inafukuzana na fuso nyingine na ghafla walijikuta wakiwa wameshapinduka

Kulia ni kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel akichukua maelezo kutoka kwa askari wa usalama barabarani



Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel akizungumza na waandishi wa habari hivi punde-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Watu 3 wamekufa na wengine zaidi ya 47 wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kwenda mnadani kupinduka wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga.

Ajari hiyo imetokea  asubuhi katika eneo la uchunga wilayani humo baada ya gari hilo haina ya fuso namba T680 ARL kuacha njia na kupinduka.

Chanzo cha ajari hiyo ni mwendo kasi na derava wa gari hilo aliyetambulika kwa jina la Shija Ngassa amekimbia  baada ya ajari hiyo

Ajari hiyo ya fuso imesababisha vifo vya watu watatu ambapo moja ametambulika kwa jina la Difa Shimo  mili ya marehemu imehifadhiwa kwenye hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Shinyanga kamishina msaidizi wa polisi Jastus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa ajari hiyo.

Kamugisha amesema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo pamoja na kumsaka dereva wa gari hilo sanajali na kutoa onyo kwa wafanya biashara wa minadani kuacha kupanda magari ya mizigo
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top