Majeruhi Adam Rashid akiwa amelazwa katika Hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam kwa majeraha ya maji ya moto.
MWANAMKE mmoja
aliyejulikana kwa jina la Fatuma Said mkazi wa Kitunda, Ilala jijini
Dar es Salaam anashikiliwa na Polisi baada ya kummwagia maji ya moto
mumewe sehemu za siri na tumboni kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa
kimapenzi, tukio lililotokea Julai 16 mwaka huu, huko Kitunda.Chanzo
chetu cha habari kililiambia gazeti hili kuwa tukio hilo lilitokea saa
12.30 jioni baada ya mwanaume huyo, Adam Rashid ambaye ana wake wawili,
kwenda katika nyumba anayoishi mke mkubwa akiwa ameandamana na mke
mdogo, kwa lengo la kupata maji ya kuoga na kubadili nguo, akitokea
kituo kidogo cha Polisi Stakishari, ambako aliwekewa dhamana kwa shauri
lililokuwa likimkabili.
Majeraha ya maji ya moto aliyopata Bw. Adam Rashid.
Inadaiwa
kuwa baada ya kuwekewa dhamana hiyo, Adam na mkewe mdogo, Aisha Juma,
waliamua kwenda nyumba anayoishi mke mkubwa, ambayo inamilikiwa na
mwanaume huyo, kwa ajili ya kuoga na kubadili nguo, wakiamini kuwa
kusingekuwa na matatizo yoyote kwa vile wanawake wote wawili anaishi nao
kihalali na wanafahamiana.
Inasemekana
kuwa baada ya kufika nyumbani hapo, Adam alimtaka mwanaye kumwandalia
maji ya kuoga na akimaliza apewe bukta, ili aweze kuondoka na mke mdogo
kuelekea wanakoishi, lakini wakati hayo yakifanyika, bi mkubwa alianza
kutoa maneno machafu ya kejeli, yaliyoonyesha wazi kuwa alikuwa na wivu
wa kimapenzi
Baada ya
mwanaume huyo kumaliza kuoga na kutoka nje, inadaiwa mkewe mkubwa
alijitokeza akiwa amebeba sufuria iliyokuwa na maji ya moto, yanayodaiwa
kuwa yalitakiwa kutumika kwa ajili ya kupikia wali na kumwagia tumboni
na sehemu za siri, huku akiendelea kumtolea maneno ya kashfa.
MAJERUHI ALONGA NA UWAZI
Akiwa
amelazwa katika wodi namba tatu kwenye hospitali ya Amana, Ilala jijini
Dar es Salaam, majeruhi Adamu Rashid alisema Julai 16 mwaka huu
alienda nyumbani kwake akiwa ameandamana na mke wake mdogo, lakini
akashangazwa na kitendo cha bi mkubwa kuanza kubwata na kumwuliza
alichokifuata, kana kwamba amesahau kama pale ni kwake na wote ni wake
zake.
“Baada ya
kunimwagia maji, mke wangu mdogo alilia sana kwa uchungu, majirani
wakanichukua na kunipeleka Polisi ambako tulimkuta bi mkubwa akiwa
anaandikisha maelezo kuwa mimi nimempiga, kuona vile askari walimgeuzia
kibao na kumwingiza ndani kwa ajili ya mahojiano zaidi.”
MKE MDOGO NAE
“Ndugu
mwandishi, mimi na mume wangu tulienda hadi kwa mke mkubwa bila
wasiwasi maana na mimi pale ni kwangu kwa sababu nyumba ya
mume wangu halali, lakini tulipofika tuliambulia maneno machafu na
kejeli.
Mke
mkubwa alihoji kwa jeuri kitu gani tulichokifuata pale, mume wangu
alikuwa akimjibu kuwa hapa nipo kwangu na huyu niliyekuja naye ni mke
wangu halali, mbona unanifanyia mambo ambayo siyaelewi, yule hakuelewa,
aliendelea tu na maneno yake machafu.”
KAMANDA WA POLISI
Kamanda
wa polisi mkoa wa kipolisi Ilala, SACP Marieth Minagi amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa huyo anashililiwa katika
kituo cha polisi Wilaya ya kipolisi Ukonga na amefunguliwa jalada na
kupewa namba RB/STK/9438/2014 KUJERUHI na uchunguzi unaendelea.
Post a Comment