Kwa mara ya kwanza wagonjwa wa kisukari nchini Senegal wameanza
kupokea ujumbe wa simu ukiwataka kufunga kwa kipindi cha kabla, wakati
na baada ya mwezi wa Ramadhan.
Senegal imekuwa nchi ya kwanza kuanza kutumia huduma hiyo ya simu
kuwasaidia wagonjwa kisukari njia muhimu na salama za kuweza kukabiliana
na kulinda afya zao haswa katika kipindi hiki cha mfungo.
Wagonjwa walioanza kupokea huduma hiyo wanasema inawasaidia sana.
Marie Gadio, mwenye umri wa miaka 26, ambaye aligundulika kuugua
ugonjwa wa kisukari akiwa na miaka 13 anasema kuwa kukabiliana na
ugonjwa huo kipindi cha mwezi wa Ramadhan sio kitu rahisi.
Post a Comment