Makamu Mwenyekiti Uenezi CHADEMA, Kanda ya Magharibi, Deogratius Liyunga akiwa amelazwa katika Hospital ya Mkoa wa Kigoma (Maweni) baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana
WATU
wasiojulikana wamemvamia na kumpiga pamoja na kumjeruhi sehemu
mbalimbali za mwili kwa kutumia vitu vyenye ncha kali Makamu Mwenyekiti
wa uenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya
Magaharibi, Deogratius Liyunga na kupelekea kulazwa katika Hospita ya
Mkoa wa Kigoma (Maweni).Tukio hilo
limetokea jana majira ya saa tano usiku katika eneo la Mlole Manispaa
ya Kigoma Ujiji,wakati kiongozi huyo akiwa njiani kurudi nyumbani kwake
akitokea eneo la Mwanga kuangalia mechi za kombe la Dunia.
Akiongea na
mtandao huu wodini na alipolazwa juu ya tukio hilo,kiongozi huyo alisema
kuwa alibakiza hatua 25 iliaweze kuingia nyumbani kwake ghafla
walitokea watu wanne,mmoja alimvamia na kumkaba shingo huku wale wengine
wakimshambulia kwa kisu,nyembe na ubao.
Alisema mbali
ya watu hao kumpiga na kumjeruhi lakini walimpora fedha kiasi cha
shilingi 63,000 ingawa hawakufanikiwa kumpora simu yake ya mkononi
iliyokuwa mfukoni.
Baada ya watu
hao waliomvamia kuondoka alifanya mawasiliano kwa watu wake wa karibu
wakiwemo wanachama wa CHADEMA ambao walifika eneo la tukio na kumkimbiza
Hospital kwaajili ya matibabu.
Makamu
Mwenyekiti alisema kuwa tukio hilo lililomkuta linahusiano mkubwa na
masuala ya kisiasa kwani kabla ya tukio hilo amekuwa akipokea ujumbe
mfupi wa maneno ya vitisho kwenye simu yake ya mkononi kutoka kwa watu
wanaodaiwa kuwa ni wananchama wa chama kipya cha ACT.
Kamanda wa
polisi wa Mkoa wa Kigoma,Frasser Kashai alipopigiwa simu na mtandao huu
kuthibitisha juu ya tukio hilo alisema hana taarifa zozote kuhusiana na
tukio hilo.
''Mimi hiyo taarifa sijaipata ofisini kwangu bado ndo nina isikia kutoka kwako ngoja nifuatilie nitakujulisha'' alisema Kashai.
Post a Comment