|
Na Shakoor JongoSIRI imefichuka! Kwa muda mrefu
mwigizaji ambaye pia ni msanii wa muziki wa mwambao, Zuwena Mohammed
‘Shilole’ amekuwa akinukuliwa akisema kuwa ana mtoto mmoja lakini sasa
mambo hadharani, ukweli ni kwamba ana watoto wawili. Kwa mujibu wa
mtu wa karibu wa familia ya staa huyo aliyepo mkoani Tabora anakotokea
Shilole, watu wanaomjua wamekuwa wakisikitishwa na matamshi yake kuwa
ana mtoto mmoja. “Tumekuwa tukisoma na kumsikia akisema ana mtoto
mmoja anayeitwa Rahma, lakini ukweli ni kwamba ana mwingine anayeitwa
Joyce na wote kazaa na wanaume tofauti,” alisema ‘sosi’ huyo kutoka
mkoani humo. Ili kupata mzani wa habari hiyo, The Biggest IQ, Ijumaa
Wikienda lilimtafuta Shilole na baada ya kumpa mkanda mwanzo, mwisho,
alikiri kuwa ana watoto wawili. “Ni kweli nina watoto wawili, Rahma
na Joyce, wote wanasoma The Click International School,” alisema Shilole
na alipoulizwa kwa nini amekuwa akisema ana mtoto badala ya wawili,
alikosa jibu. |
on Saturday, July 5, 2014
Post a Comment