Mtoto Mwenye Umri wa Miezi Minne Celin
Kyando Amefariki Dunia Baada ya Chumba Alichokuwa Amelala Kuteketea na
Moto Katika Mtaa wa Buguruni Mjini Njombe Wakati Mama Yake Rose
Luambano Akiwa Bafuni Anaoga.
Mtandao huu Umefika Eneo la Tukio
na Kuzungumza na Baadhi ya Mashuhuda Ambao Wamesema Kuwa Tukio Hilo
Limetokea Majira ya Saa Sita Mchana Julai Sita Mwaka Huu na Kuongeza
Kuwa Chanzo cha Ajali Hiyo ya Moto ni kifaa cha umeme kitumikacho kupashia maji (Hita) ambayo iliachwa bila ya kuzimwa.
Hati Hivyo Mashuhuda Hao Kwa
Kushirikiana na Wananchi wa Mtaa wa Buguruni Wamefanikiwa Kuzima Moto
Huo Kabla ya Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Pamoja na Jeshi la Polisi
Kufika Eneo la Tukio , Huku Baadhi ya Wapangaji Wengine wa Nyumba Hiyo wenye maduka
Wakionekana Kuhamisha Mali Zao Kwa Hofu ya Kuungua.
Tukio hilo lililotokea
kwenye Nyumba ya Bw. Danfoard Mhelela yenye Namba za Usajili MTW 94
ambapo Licha ya kufariki dunia kwa mtoto huyo lakini pia vitu mbalimbali
vimeteketea kwa moto.
Wameleza Kuwa Baada
ya Jeshi la Polisi Kufika Eneo la Tukio Limeuchukua Mwili wa Mtoto Huyo
Pamoja na Wazazi Wake na Viongozi wa Mtaa Huu na jududi za kupata uthibitisho kutoka kwa jeshi la polisi bado zinaendelea.
Mwenyezi mungu ailaze roho ya mtoto celin mahala pema peponi.
Na James Festo, hfesto blog Njombe.
Post a Comment